Na John Richard Marwa
Klabu ya Yanga imezidi kujikita katika maandalizi ya kuelekea mchezo wa pili kuwania kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC dhidi Club Africain ya Tunisia.
Yanga ambayo ilitua jana nchini Tunisia imeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo huo wa kufa ama kupona unaotarajiwa kufanyika November 9 Mjini Tunis.
Akizungumza na Sports Extra ya Clouds Ofisa Habari wa Yanga Ally Kamwe amewataka mashabiki,wananchama na wapenda soka kuendelea kuiombea klabu yao iendelee kuwa katika hali nzuri ambayo itawafanya kuweza kafanya vizuri.
"Tuko salama na kikosi jana kilifanya mazoezi ya kuweka miili sawa na leo muda huu tayari timu iko Uwanjani kwa awamu nyingine ya mazoezi"
"Hali ya hewa ya huku ni ya baridi kwa sasa ni nyuzi joto 15°c, jana iliwapa tabu kidogo wachezaji lakini wanasema ni hali nzuri ambayo itawafanya kuweza kukimbia muda wote wa mchezo ikishazoeleka mwilini.
Kuhusu wapenda soka wa Tunisia nini wa wanakizungumzia kuhusu Yanga Ally anasena.
"Jambo la kufurahisha ni kuwa wanawafahamu wachezaji wetu, wamekuja hotelini wakimuulizia Mayele, Aziz Ki ni jambo la kutia Moyo.
"Lakini kwa namna wanaizungumzia Club Africain wanasema Club Africain inapitia wakati mgumu mara baada ya kufungiwa kusajili na FIFA hivyo kikosi chao bado kinajitafuta." amesema Ally Kamwe.


No comments:
Post a Comment