November 08, 2022

CHAMA, AZIZ KI WAPIGWA NYUNDO NPL



Na Mwandishi Wetu


Viungo washambuliaji wa Klabu za Simba na Yanga Clatous Chama (Simba SC) na Stephan Aziz Ki (Yanga SC) wefungiwa kutocheza michezo mitatu ya Ligi Kuu Soka Tanzania Bara NPL na faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kila mmoja.

Adhabu hizo zimetokana na kukutwa na kosa la kukwepa kusalimiana na wachezaji wa timu pinzani kablà ya kuanza kwa mchezo ulioikutanisha klabu hizo Oktoba 23, 2022.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Uendeshaji na usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania TPLB katika kikao chake cha Novemba 4, 2020 imebainisha kuwa.

"Wachezaji hao kwa nyakati na mazingira tofauti walionekana kufanya hila kwa kusubiri nje ya kiwanja ili zoezi la kusalimiana likamilike ndipo waingie kiwanjani"

"Adhabu hii ni kwa uzingativu wa kanuni 41:5(5,4) ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti kwa wachezaji." Imeeleza taarifa hiyo.

Ikumbukwe kuwa mchezo huo ulimalizika kwa miamba hiyo kutohana nguvu kwa sare ya bao (1-1), Simba wakifunga kupitia kw Agustin Okrah huku Yanga wakisawazisha kupitia kwa Stephan Aziz Ki.



No comments:

Post a Comment

Pages