November 15, 2022

KILANGO AANZISHA MRADI SAME MASHARIKI

 

Mbunge wa Same Mashariki, Anne kilango, akizungumza na wananchi wa jimbo lake.


 
 

Na Mwandishi Wetu


Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango ameanzisha miradi ya viti vya kukodisha kwa ajiri ya biashara kwenye kata 14 katika jimbo lake la Same Mashariki ambazo kila kata zimepatiwa viti 100.

Amesema hatakikisha pesa hizo zitawasaidia kwenye kampeni za wenye viti wa kitongoji na vijiji ifikapo mwaka 2024    kusiwe na changamoto yoyote ya kipesa wakati wa kampeni.
 
 
Pia amewagiza Madiwa kutunza  mradi huo wa kukodisha viti hili huwe chachu ya maendeleo katika serikali za mitaa lengo ni kuwanadi vingozi wao wa chama cha mapinduzi.
 

Mhe Anne kilango amesisitiza kata itakayofanya vizuri 2023 atawaongezea mradi mwingine hili wajikite kutengeneza pesa ambazo zitawanufaisha kwenye chaguzi ndogo ndogo na kuondoka na dhama za kuomba omba pesa za kampeni.
 

Aliendelea kusema lengo la kuanzisha miradi hii pia ni moja ya kutekeleza Ilani ya chama cha mapinduzi kukisaidia chama cha mapinduzi kushinda chaguzi zote za serikali ya mtaa na uchaguzi mkuu ambao utafanyika August 2025.
 

Pia Mhe Anne kilango ametoa shukran za dhati kwa muheshimiwa Raisi Samiha Suhuru Hassani kwa kumpatia Fedha za kutosha kwa ajiri ya ujenzi wa barabara zote za Same Mashariki ambazo barabara hizo sasa hivi wameshakabidhiwa wakandarasi na zinafanyiwa kazi.
 

Kilango pia ametoa wito kwa watanzania kwa ujumla kumuunga mkono muheshimiwa Raisi Samiha Suhuru Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya kuijenga nchi kwenye kila nyanja tofauti michezo barabara Upatikanaji wa maji safi na salama na kujenga hospital za kisasa na kadharika  picha na (Ashrack Miraji).

No comments:

Post a Comment

Pages