Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary
Masanja, akifungua Warsha ya 22 ya
Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) katika ukumbi wa
Mikutano wa EDEMA Mkoani Morogoro leo.
Na Mwandishi Wetu
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja, amewaasa wadau wa
misitu kote nchini washiriki kikamilifu katika usimamizi na utunzaji wa
maeneo ya misitu ya vijiji ili kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi.
Ameyasema
hayo leo Novemba 15, 2022 wakati wa ufunguzi wa warsha ya 22 ya Mtandao
wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA)mkoani Morogoro.
"Kasimamieni
misitu vizuri msigawe maeneo hovyo, mkaweke mpango wa matumizi bora ya
ardhi ili kuzuia uvamizi kwenye maeneo ya hifadhi" Mhe. Masanja
amesisitiza.
Aidha, amewataka viongozi wa MJUMITA wawaelimishe wananchi juu ya usimamizi wa misitu na umuhimu wa uhifadhi.
Katika
hatua nyingine Mhe. Mary Masanja amewataka viongozi hao wakemee mila
potofu ambazo zinamkandamiza mwanamke na kumnyima fursa za kushiriki
kwenye uhifadhi wa misitu .
'Tuchukue
hatua mara moja kuhakikisha jinsia inazingatiwa ili kulinda misitu yetu
na kuhakikisha jamii inanufaika na uwepo wa Misitu hiyo" ameongeza.
Aidha,
amesisitiza kuwa misitu ikisimamiwa vizuri ina uwezo mkubwa wa
kudhibiti mabadiliko ya tabia ya nchi, kutunza vyanzo vya maji, kuwa
makazi ya wanyama hai na chanzo cha mapato kwa jamii hasa kwa kutekeleza
shughuli za ufugaji nyuki.
Lengo
la warsha hiyo ni kujenga uelewa wa pamoja wa dhana za ujumuishi wa
wanawake na vijana katika uhifadhi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia
ya nchi, kubadilishana uzoefu wa namna ya kutekeleza dhana ya ushiriki
wa jinsia kwenye uhifadhi wa misitu, kujadiliana kuhusu fursa na
changamoto zinazowakabili wanawake na vijana katika uhifadhi na ushiriki
katika mnyororo wa thamani ya mazao ya misitu.


No comments:
Post a Comment