Kocha
Mkuu wa klabu ya Simba Juma Mgunda amesema kuwa Ligi ni ngumu lakini
wataendelea kuapmabana hadi mchezo wa mwisho wa msimu.
Mgunda
ameyasema hayo mchana wa leo katika Mkutano na Waandishi wa Habari
kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Namungo FC, mtanange utakao chezwa
kwenye Dimba la Benjamin Mkapa.
Ameongeza kuwa bado wako kwenye mbio za Ubingwa hivyo Mapambano yanaendelea hadi mwisho.
"Nikiri kwamba Ligi ni ngumu na itaendelea kuwa ngumu, kikubwa kwetu ni kuendelea kupambana mpaka mwisho."
"Bado tupo katika kuwania ubingwa na mpaka tuakapocheza mechi ya mwisho ndio bingwa atafahamika " amesema Mgunda.
Simba wametoka kupata ushidi kiduchu dhidi ya Ihefu FC wa bao moja kwa mtungi.
Kuelekea mchezo huo Simba wanaendelea kumkosa Peter Banda ambaye atakuwa nje ya Dimba kwa miezi miwili.


No comments:
Post a Comment