Meneja wa Biashara wa Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar, Bi. Naima Shaame (kushoto), akizungumza katika warsha maalum ya Benki ya NMB pamoja na wakandarasi iliyolenga kuzitambulisha suluhisho mpya za benki ya NMB kwa wakandarasi. Katikati ni Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano a Uchukuzi, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohamed, wapili kulia ni waziri wa Ardhi, Mhe. Rahma Kassim Ali, kulia ni naibu waziri wa Ardhi, Mhe. Juma Makungu Juma na wapili kushoto ni Mkuu wa Idara ya Miamala ya Benki ya NMB, Bi. Linda Teggisa.
Na Mwandishi Wetu
Wizara
ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi -Zanzibar imeipongeza Benki ya NMB
kwa kuleta masuluhisho maalum yalio rafiki kwaajili ya wakandarasi huku
akiamini ndio njia rahisi ya kusaidia kuwakuza wakandarasi wazawa
kiuchumi.
Hayo yamesemwa
na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, Mhe. Dkt. Khalid Salum Mohammed alipokuwa anazindua rasmi
warsha ya Benki ya NMB pamoja na wakandarasi wa Zanzibar ikiwa na lengo
la kuwatambulishia suluhisho mpya kwaajili ya wakandarasi na kuwasihi
wachangamkie fursa hizo.
Mbali
na hilo, Waziri huyo aliwasihi pia wakandarasi kutumia fedha za mikopo
wanaopata kutoka kwa mabenki kwaajili ya kazi waliokopea na sio kwa
shuguli zingine kwa inaweza wapa ugumu katika kurejesha mkopo huo.
Akizungumza
katika warsha hiyo, mwakilishi wa Benki ya NMB ambae ni Mkuu wa Idara
ya Miamala wa Benki hiyo, Bi. Linda Teggisa alisema kuwa Benki ya NMB
imesimama katika nafasi ya kuendelea kuongeza fursa ya upatikanaji wa
huduma za kifedha ili kuendelea kuwawezesha wakandarasi kutekeleza
miradi mbalimbali ikiwemo utoaji wa huduma za dhamana za zabuni kwaajili
ya miradi au manunuzi (unsecured bid bond) pamoja na dhamana za
utekelezaji (performance guarantee) au dhamana za malipo ya awali
(advance payment guarantee), zote ambazo hazihitaji dhamana.
Akizungumza
kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibu, Mkuu wa wilaya ya Mjini,
Mhe. Komred Rashid Simai Msaraka alisema kuwa sekta ya ujenzi imekuwa ni
sekta ya muhimu sana kwa Zanzibar kwa sasa kwani ni miongoni mwa Sekta
ambazo zinaongeza ajira zilizo na zisizo rasmi kwa wananchi wa Zanzibar
na kupongeza taasisi za fedha kuamua kuongeza nguvu kwa sekta hii sio tu
kuwanyayua wakandarasi lakini linaenda kupunguza changamoto ya
upatikanaji wa ajira kwa Zanzibar.



No comments:
Post a Comment