November 03, 2022

SIMBA QUEENS WAANZA KAZI MOROCCO




Na John Richard Marwa

Kikosi cha Simba Queens wamepata ushidi wa kwanza dhidi ya Determine Girls ya Liberia wa mabao (2-0) mchezo wa pili hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Soka la Wanawake ngazi ya klabu Barani Afrika.

Simba Queens waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya AS Far ya Morocco kwa (1-0).

Mchezo huo ulianza kwa timu zote kuwa nidhamu katika maeneo ya uwanja hali iliyopelekea dakika 45 za kwanza kutamatika kwa suluhu.

Kipindi cha pili Simba Queens waliingia kwa kushinikiza mashambulizi na kujipatia mabao (2-0) kupitia kwa Oppah Clement na Olaiya Barakat.

Ushindi huo umeifanya Simba Queens wamejiweka kwenye nafasi nzuri ya kuwania kutinga hatua ya Nusu Fainali kama itafanikiwa kushinda mechi ya mwisho ya hatua hiyo ya makundi.

Licha ya ushindi huo Simba Queens wamekosa makali katika safu yao ya ushambuliaji wakikosa nafasi nyingi sana kwa mechi mbili za awali walizocheza hadi sasa.
 

No comments:

Post a Comment

Pages