Na Mwandishi Wetu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF wameingia mkataba wa udhamini na kampuni ya usafirishaji wa Anga Precision Air wenye lengo la kutoa usafiri kwa viongozi katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Kwa mujibu wa pande mbili za mkataba huo ultakuwa na thamani ya Tsh million 108 kwa msimu mmoja.
Wakati huo huo Rais wa (TFF), Walace Karia amesema wapo kwenye mazungumzo na kampuni mbalimbali kwa ajili ya udhamini wa Kombe la TFF ama ASFC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Karia amesema kombe hilo halina mdhamini mkuu na hata kuitwa kombe la Shirikisho Azam ni kutokana na kutokuwa na mdhamini mwingine.
“Kombe linaitwa Azam kwa sababu tulisaini nao mkataba wa kuonyesha matangazo kwahiyo hakuna mdhamini mwingine ndio maana,” amesema Karia na kuongeza;
“Akitokea mdhamini mkuu basi jina lake litakaa pale, halafu hata kuitwa hilo jina ambalo linaitwa sasa ni kukosea maana jina lake ni kombe la TFF.”
Karia amesema wapo kwenye mazungumzo na baadhi ya kampuni kwa ajili ya kudhamini kombe hilo na akipatikan basi mdhamini jina lake litasimama kwenye Kombe rasmi.


No comments:
Post a Comment