Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika Hafla ya Utiaji Saini wa mkataba huo, Mkurugenzi Mkuu wa
TRC,Mhandisi Masanja Kadogosa amesema kuwa mitambo na mashine hizo ambazo
zitakuwa zaidi ya 26 zenye thamani ya dola za kimarekani milioni 51
zitaendeshwa kisasa kulingana na kiwango cha reli ya kisasa
inayomalizika kujengwa hapa nchini kufanya matengenezo ya reli hiyo
pindi itakapoanza kufanya kazi.
Amebainisha kuwa mkataba huo ni Sehemu mojawapo ya kuelekea katika mchakato wa
kuanza rasmi kwa uendeshaji wa kutoa huduma za usafirishaji wa treni ya
SGR mpaka kufikia mwezi Aprili 2023.
Amesisitiza kuwa
kuwa lengo la ununuzi wa mashine na mitambo hiyo ni kuongeza ufanisi wa
matengenezo ya njia na kupunguza kufanya matengenezo ya njia kwa
kutumia watu ambapo mitambo hiyo italipa uwezo shirika katika kutunza
reli hiyo ya kisasa ya SGR.
Ameongeza kuwa utekelezaji wa mkataba huo ambao utahusisha
utengenezaji,mafunzo, makubaliano na makabidhiano unatarajiwa kufanyika
kwa miezi 12.
Amefafanua kuwa nauli za treni hiyo ya kisasa itakayotumia umeme katika uendeshaji
wake, Masanja amewaondoa hofu watanzania kwa kusema kuwa nauli hizo
zitaendana na mahitaji ya watanzania na zitakuwa nafuu kwao ambapo kwa
sasa watazunguka katika mikoa mbalimbali kuzungumza na wananchi pamoja
na wadau mbalimbali juu ya kupanga kiwango cha nauli hizo kutokana na
watakavyokubaliana nao wakishirikiana na mamlaka ya usafiri wa ardhini
Latra.
"Niwahakikishie
watanzania kwa bei ambazo tutakuja nazo kila mtanzania ataweza kuzimudu
na zitaendana na mahitaji ya watanzania na tumejipanga kwa hilo
kuhakikisha tunatoa huduma bora na za kisasa katika mradi huu wa treni
ya mwendokasi (SGR)"amesema Kadogosa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo, John Kandoro amesema
kuwa mitambo ambayo itanunuliwa na shirika hilo kupitia mkataba huo
uliosainiwa hii leo utasaidia shirika hilo kuachana na matumizi ya
kizamani ya njia za reli (washika vibendera)na kuja na matumizi ya
kiteknolojia ambayo yatakuwa mwarobaini wa sekta ya usafirishaji kwa
njia ya reli mchini na yatachangia TRC kuendeshwa kisasa.
Pia amesema kuwa mitambo hiyo itaendana na reli mpya ya kisasa na
kuongeza kuwa kampuni ya (SSRST) itakuwa ikisaidia Sehemu ya marekebisho
ya reli ya kisasa kupitia mitambo hiyo sambamba na kutoa mafunzo ya
kutumia mitambo hiyo kwa wahandisi na mafundi wa kitanzania ili kuongeza
ufanisi wa matumizi yake.
Hata
hivyo amesema bado shirika litaendelea kutoa huduma za usafirishaji wa
reli kupitia treni za reli ya kawaida ambazo zinaendelea kutoa huduma
hivi sasa.
Nae, Balozi wa Korea
Kusini nchini, Kim Sun Pyo amesema kuwa anataegemea mkataba huo utaleta
matokeo ya kisasa mradi wa SGR ukikamilika na kuipandisha kiuchumi
Ukanda wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkataba wa
makubaliano hayo baina ya shirika la reli Tanzania TRC na kampuni ya
Sung Shin Rolling Stock Technology SSRST ya nchini Korea umesainiwa
mbele ya viongozi mbalimbali wa Shirika hilo na Makamo wa Rais wa
kampuni ya SSRST, K.Charles Park na Balozi wa nchi ya Korea kusini hapa
nchini,Balozi Kim Sun Pyo.



No comments:
Post a Comment