Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya Kidato cha Nne ya shule 11 za kiislamu mkoani Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imewataka walimu, shule kuzingatia maadili na malezi bora kwa wanafunzi.
Akizungumza katika
mahafali ya Kidato cha Nne ya shule 11 za kiislam zilizopo mkoani wa
Dar es Salaam Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda
amesema.
"Natoa wito kwa wenye shule na walimu, wenye shule ni pamoja na serikali, shule nyingi ziko tamisemi ziko serikalini, lakini nyingine za watu binafsi, nyingine za makanisa zingine za kiislamu zote hizo tunapenda kutoa wito kwa walimu na wenye shule wasimamie malezi ya vijana. Watumie bidii zote kuhakikisha kwamba suala la malezi na maadili ni suala muhimu Sana."
"Walimu tunakazi ya kuwasaidia wazazi, na walimu tunafanya kazi nzuri labda niseme hivi, wanasema samaki mmoja akioza wote wameoza lakini itakuwa bahati mbaya sana kudhani kuwa walimu wetu hawafanyi kazi ila ni ukweli kwamba wanafanya kazi nzuri sana." amesema na kubainisha kuwa.
"Na sisi tusingependa Mwalimu mmoja ama wawili au shule moja ikaacha kusimamia malezi bora na maadili kitu ambacho kitawaharibu vijana wetu wote. Kwa hilo tutalisimamia na tutaongeza bidii na nina laani vikali sana wale walioruhusu ule mchezo wa shule hizo waliokutana shule mbili pale kisarawe mchezo waliokuwa wanaufanya na picha zikapigwa haiwezekani walimu wakawa hawakujua na hapo pekee tumeona kipande hicho cha video, tukishafanya uchunguzi imekuwa ni kawaida ya kuwaachia kujiachia hairuhusiwi na tuna laani sana vitendo vile na tunajitahidi kuhakikisha kwamba tutachukua hatua zaidi kwa pale ambapo tutajua kilichotolea leo kilichotokea juzi lakini vyote hivyo havikubaliki." Prof Mkenda amesema.
"Na hilo swala la maadili linaenda hadi kwenye kusimamia mitihani hata katika kufundisha darasani kuhakikisha kwamba tunatumia haki, tunafanya vizuri, tunachokifundisha darasani ndicho ambacho tunachotaka wakifane maishani. Tukiwafundisha kwenye mtihani kuibiana tunawafindisha kwenye maisha twende tukaibe hata akifanya vizuri akikabidhiwa Ofisi ya serikali akawa mwizi basi tunakuwa tumechangia kuleta uharibifu huo."
"Lakini zaidi ya hayo kuna mmomonyoko wa kimaadili ambao ni makoa ya jinai yapo, Kuna visa vya baadhi ya walimu wachache sana kujaribu kutafuta mahusiano na wanafunzi, watoto, hukumu inafahamika sisi tutafuatilia na hata sasa hivi nafuatilia kesi moja, tutafuatilia waendesha mashtaka wayasimamie mashtaka haya vizuri hao wote mabalazuri wanaotaka kuharibu vijana wetu watoto wetu wahukumiwe wafungwe kuhakikisha kwamba tabia hizi zinakomeshwa na wanaofanya hizi wanaadhibiwa wanakoma" Prof. Adolf Mkenda.




No comments:
Post a Comment