Na Happiness Katabazi, Liwale
MGANGA Mfawidhi wa Wilaya ya Liwale Mkoani Lindi, Gloria Andrew amesema Halmashauri ya wilaya Hiyo imepokea Sh 750,000,000 kwaajili ya ujenzi wa majengo manne ya Hospitali mpya ya wilaya ya Liwale ikiwa ikiwa ni utekelezaji wa ujenzi wa awamu ya nne.
Dr. Gloria aliyasema hayo juzi wakati akisoma taarifa ya ujenzi wa Hospital mpya ya wilaya katika Kijiji Cha Liwale 'B' kwa Mbunge wa Jimbo la Liwale Zuberi Kuchauka na Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo Milingo Kindamba ambao walifanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
Alisema Halmashauri ilipokea kiasi hicho Cha fedha Oktoba 21 mwaka huu kwaajili ya ujenzi wa majengo sita ambayo ni wodi tatu ( wodi ya watoto,wodi mbili za magonjwa ya mchanganyiko wanaume na wanawake) na jengo la kuhifadhia maiti Kwa chanzo Cha serikali Kuu na na kuwa ujenzi ulianza Desemba 12 mwaka huu na unatarajia kukamilika Machi 2023.
Dr. Gloria alisema kiasi Cha sh 140,957,221.5 zimepitishwa na kamati ya fedha kuwa zitatoka kwenye mapato ya ndani kwaajili ya kukamilisha majengo yote sita ambalo ni jengo la Utawala, Wazazi,Bohari ya dawa,mionzi,jengo la kufulia na Jengo la dharula na kwamba umaliziaji wa majengo hayo utategemea upatikanaji wa fedha za mapato ya ndani.
Aidha alisema ujenzi wa awamu ya kwanza wa majengo ya mawili ya OPD na maabara ulianza mwaka 2020 na kwamba majengo yamekamilika na yameanza kutoa baadhi ya huduma .
Kwa upande wake Mbunge wa Liwale, Zuberi Kuchauka alisema ameridhika na hatua za ujenzi na akawashauri wajenzi watumie taaluma zao kujenga majengo Bora na akapongeza jitihada za serikali kutoa fedha za kujenga hospital ya kisasa wilayani mwake
Na wananchi mbalimbali walipongeza jitihada za serikali za kuleta fedha za kuwangea wananchi wa Liwale Hospitali ya Kisasa.
CHANZO: Gazeti la Habari Leo Desemba 30, 2022.
No comments:
Post a Comment