January 31, 2023

Benki ya Maendeleo yapata faida zaidi ya mara mbili Mwaka 2022

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam


Benki ya Maendeleo (Maendeleo Bank Plc) imesema kuwa imefanikiwa kupata faida zaidi ya mara mbili huku ikibainisha katika kipindi cha mwaka 2021  kupata faida kutoka   Sh Milioni 587 hadi Sh Bilioni 2.02 kwa mwaka 2022.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Dkt. Ibrahim Mwangalaba amesema  ongezeko hilo ni sawa na Asilimia 184 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 163 ongezeko hilo limetokana thamani ya hisa 50 za benki.

"Kabla ya Faida na baada ya Faida Ukuwaji wa wanahisa umeongezeka kwa Asilimia 8, Faida kabla ya Kodi imeongezeka kutoka Milioni 710 hadi kufikikia billion 2.2 kwa Mwaka 2022 wakati Faida baada ya Kodi imeongezeka kutoka shilingi Milioni 587 Hadi kufikikia Shilingi bilion1.3122 kwa Mwaka ". Alisema Dkt. Mwangalaba.

Aidha Dkt Mwangalaba aliongeza kuwa ukuwaji wa mapato hayo umetokana na ukuaji wa mapato kwa Asilimia 22 kutoka bilioni 7.6 kwa Mwaka 2021hadi kufikia shilingi Billion 9.9

Amebainisha kuwa hali ya Kibiashara ya mikopo imeweza kuimarika kutoka mikopo chechefu ya Asilimia 13 kwa kipindi cha mwaka 2021 hadi kufikikia 5.2 mwaka 2022 hali iliyochangiwa na mapato ya taasisi hiyo.

"Amana za wateja ziliongezekakwa Asilimia 11 kutoka billion 70 Mwaka 2021hadi bilioni 77". Ameongeza Dkt. Mwangalaba.

Dkt Mwangalaba amesema benki hiyo inamtaji wakutosha na wanatazamia kufanya kazi nchini kote ikiwemo kuongezeka tawi moja katika eneo la Mbagala kabla ya mwezi wa nne, kuanzisha huduma za kimtandao,(Internet Benking) pamoja na kuanzisha mfumo wa ulipaji ada ambao utapeleka taarifa papo hapo kwenye shule husika pindi mzazi atakapolipa ada kupitia benki hiyo na kuondoa usumbufu wa kupeleka risiti shuleni.

Kuhusu mikopo Dkt Mwangalaba amesisitiza kuwa kwa mwaka 2022 benki hiyo imeshakopesha wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga 2500 kwa kuwapatia mikopo iliyofikia Sh Bilioni 3 ambao kwa kiasi kikubwa ndio waliochangia kuongezeka kwa faida ya benki hiyo.

Hatahivyo amesema kwa mwaka 2023 benki hiyo imeweka mikakati ya kuwafikia wafanyabiashara wadogo zaidi ya 5,000, vijana pamoja na makundi ya wanawake wajasiriamali

Katika hatua nyingine amesema kwa mwaka 2023 wamejipanga kuongeza tawi, kuboresha huduma za mtandao pamoja na ubunifu wa bidhaa mpya kwa wateja.

No comments:

Post a Comment

Pages