January 10, 2023

Lipumba azindua Mikutano ya Hadhara ya CUF

Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Chama cha Wananchi (CUF) kimezindua rasmi  Mikutano ya Hadhara ambapo umeudhuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Profesa Ibrahim Lipumba Katika Viwanja vya Bakhresa Mazenze, Wilayani Ubungo jijini  Dar es Salam.

 

Mkutano huyo ulioudhuriwa  na mamia ya wananchi, viongozi  wa chama pamoja na wafuasi wa chama hicho kutoka maneno mbalimbali ya jiji.

Akizungumza katika mkutano huo  Mwenyekiti  wa CUF  Profesa  Iblahim Lipumba amesema wamezindua mikutano yao ambayo itafanyika nchi nzima Kwa lengo la kunadi sera za chama na kuimarisha chama nchi nzima.

Mapema akizungumza wakati akimkaribisha mwenyekiti wa chama Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF  Taifa, Injinia Mohamed Ngulangwa amesema wakati huu ulikuwa ukisubiliwa  kwa hamu kufatia zuio lililowekwa kwa vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara katika kipindi cha zaidi ya miaka sita.

Amebainisha kuwa kipekee amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutengua na kuruhusu mikutano ya hadhara kuanza tena baada ya marufuku ililokuwepo ya mtangulizi wake Rais Magufuli kwa miaka zaidi ya sita.

"Tanzania tumepitia kipindi kigumu sana hasa vyama vya upinzani ilifika wakati baadhi ya matukio na vitendo kama vile kupotea kwa watu na kuokotwa kwa maiti pembezoni mwa fukwe vilikuwa vinaongezeka lakini kufatia jitihada za mheshimiwa rais  taifa imefikia mda viongozi wanakaa meza moja kuzungumzia maswala yanayohusu mustakabadhi wa taifa" Amesema Injinia Ngulangwa.

Injinia Ngulangwa ameongeza kuwa pamoja na changamoto ambazo kama taifa tulizipitia kufatia zuio hilo katika kipindi chote cha miaka sita aimaanishi kuwa tushindwe kupongeza kwa mazuri yaliyofanyika ikiwa ni pamo na kukosoa kistaarabu na kushauri inapobidi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ubungo, Bashiru Muya akizungumza katika uzinduzi huo alisema mikutano hiyo ya hadhara itasaidia kujenga vyama vya siasa sambamba na kunadi sera zao kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment

Pages