Chama
cha Wananchi (CUF) kimezindua rasmi Mikutano ya Hadhara ambapo
umeudhuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Profesa Ibrahim Lipumba
Katika Viwanja vya Bakhresa Mazenze, Wilayani Ubungo jijini Dar es Salam.
Mkutano
huyo ulioudhuriwa na mamia ya wananchi, viongozi wa chama pamoja na
wafuasi wa chama hicho kutoka maneno mbalimbali ya jiji.
Akizungumza
katika mkutano huo Mwenyekiti wa CUF Profesa Iblahim Lipumba
amesema wamezindua mikutano yao ambayo itafanyika nchi nzima Kwa lengo
la kunadi sera za chama na kuimarisha chama nchi nzima.
Mapema
akizungumza wakati akimkaribisha mwenyekiti wa chama Mkurugenzi wa
Habari na Mawasiliano wa CUF Taifa, Injinia Mohamed Ngulangwa amesema
wakati huu ulikuwa ukisubiliwa kwa hamu kufatia zuio lililowekwa kwa
vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara katika kipindi cha zaidi
ya miaka sita.
Amebainisha
kuwa kipekee amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutengua na
kuruhusu mikutano ya hadhara kuanza tena baada ya marufuku ililokuwepo
ya mtangulizi wake Rais Magufuli kwa miaka zaidi ya sita.
"Tanzania
tumepitia kipindi kigumu sana hasa vyama vya upinzani ilifika wakati
baadhi ya matukio na vitendo kama vile kupotea kwa watu na kuokotwa kwa
maiti pembezoni mwa fukwe vilikuwa vinaongezeka lakini kufatia jitihada
za mheshimiwa rais taifa imefikia mda viongozi wanakaa meza moja
kuzungumzia maswala yanayohusu mustakabadhi wa taifa" Amesema Injinia
Ngulangwa.
Injinia
Ngulangwa ameongeza kuwa pamoja na changamoto ambazo kama taifa
tulizipitia kufatia zuio hilo katika kipindi chote cha miaka sita
aimaanishi kuwa tushindwe kupongeza kwa mazuri yaliyofanyika ikiwa ni
pamo na kukosoa kistaarabu na kushauri inapobidi.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ubungo, Bashiru Muya
akizungumza katika uzinduzi huo alisema mikutano hiyo ya hadhara
itasaidia kujenga vyama vya siasa sambamba na kunadi sera zao kwa
wananchi.
No comments:
Post a Comment