Na Janeth Jovin
MAENEO zaidi ya 30 yaliyopo jijini Dar es Slaam na Pwani ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili yanatarajiwa kukosa maji kwa saa 36 kutokana na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu chini uliyopo Bagamoyo kuzimwa leo Jumatatu Januari 30, 2023.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kitengo wa Mawasiliano cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) imeeleza kuwa mtambo huo utazimwa lengo ni kuruhusu kazi ya kusafisha mifumo yote ya mtambo ikiwemo machujio, matanki na mabomba makuu yote ya kusafirisha maji kutoka katika mtambo huo.
"Kutokana na kazi hiyo maeneo yanayohudumiwa na mtambo huo yatakosa huduma za maji kuanzia Jumatatu (leo) Januari 30,2023 hadi Jumanne jioni," ilieleza taarifa hiyo
Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoatjiriwa mbali na Hospitali ya Taifa Muhimbili mengine ni Mwananyamala, Kinondoni, Buguruni, Vungunguti, Ilala, Katikati ya mji,Msasani, Masaki, Osterbay, Mikocheni, Kijitonyama, Lugalo, Kawe, Makongo, Keko, Kurasini, Magomeni, Kigogo
Maeneo mengini ni Mji wa Bagamoyo, MapingaZinga, Kerege, Mabwepande, Bunju, Kunduchi, Chang'ombe, Teresa, Mbezi Beach, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Kunduchi, Mivumoni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege, Mwenge, Lugalo pamoja na Kiwalani.
Aidha taarifa hiyo ilieleza kuwa Dawasa inawaomba wananchi kukumbuka kuhifadhi maji ya kutosha ili kuweza kuyatumia katika kipindi chote cha matengenezo.
No comments:
Post a Comment