Na Lucas Raphael, Tabora
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Tabora imemuhumu kwenda jela miaka 20 Adam Frank (31) baada ya kumtia hatiani kwa kosa la usafirishaji haramu wa binadamu kinyume cha sheria.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkuu Mkazi wa Mkoa wa Tabora Gabriel Ngaeje alisema hukumu hiyo iwe fundisho kwa watu wengine wenye ni kama hiyo ya kusafirishaji wa binadamu jambo ambalo likiachiwa litaku sugu.
Alisema kuwa vitendo vya kusafirisha binadamu naona linataka kuwa kubwa hivyo sharia zipo lazima kila mtu anatakiwa kuzifuata na kuacha utumikishwaji na usafirishaji wa binadamu ukomeshwe
Alisema kwamba mtuhumiwa huyo alijulikana baada ya gari alilokuwa akisafirishia raia 3 wa Kisomali kupata ajali na kuacha njia na kupinduka katika kijiji cha Makomero Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora.
Alisema mahakama imemuona mshitakiwa kuwa na hatia kwa kosa la kusafirisha binadamu ambao ni Raia wa Kisomali Abdullahi Mohamesi {28} ,Zakaria Zekele {18} ,Deka Haile {27} kinyume cha sheria za nchi.
Hakimu Ngaeje alisema kwamba mpaka sasa Raia hao wamekwisha kudishwa kwa kwao baada ya kulipa faini ya Laki tano kila mmoja kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.
Wakili wa Uhamiaji Octavian Kilatu aliiambia Mahakama hiyo kwamba tukio hilo liltokea februal 25 mwaka jana wakati mshitakiwa alikuwa akiwasafirisha Raia hao kinyume na utaratibu wa uhamiaji ambapo dereva wa Adamu Frank akiwa anawasafirisha kwenye gari hilo mali ya Subira Charles majira ya jioni.
Wakili huyo aliambia mahakama hiyo kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kusabisha gari hilo kuacha njia kisha kupinduka na raia hao kupata majeraha na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Raia hao wa Somalia walikiri kufanya kosa hilo na kutozwa faini ya laki 5 kila mmoja na ndugu zao walifika mahakamani hapo na kutoa fedha hizo ,hivyo wamerudishwa kwao.
Katika kesi hiyo mshitakiwa alitakiwa kulipa faini ya shilingi million 20 au kwenda jela miaka 20 ambapo mshitakiwa alishindwa kulipa fedha kiasi kilichotaja na mahakama hiyo na hivyo kupelekwa jela kutumika kifungo chake .
No comments:
Post a Comment