Na Mwandishi Wetu
Kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kusafiri kesho kuelekea Dubai kikiwa na msafara wa watu 38 kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya siku saba kujiandaa na mechi za ligi kuu na mashindano mengine.
Kambi hiyo ni mualiko kutoka kwa Rais wa heshima wa klabu ya Simba Mohammed Dewji(Mo) ili kuipa nafasi timu kufanya maandalizi ya kujiandaa na michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba wakiwa Dubai wanatarajia ķucheza michezo miwili ya kirafiki ambapo ratiba kamili itajulishwa baadaye.
Kikosi cha Simba kitarejea nchini January 14, tayari kwa mchezo wao wa ligi kuu ya NBC dhidi ya mbeya City utakaopigwa January 17 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Akizungumzia kambi hiyo Robertinho amesema ni maamuzi sahihi ambayo yatampa nafasi ya kuangalia kikosi chake kwa mapana na kuanza kupandikiza falsafa zake akishirikiana na makocha wenzake Juma Mgunda na Selemani Matola.
"Ni uamuzi mzuri kwa uongozi kunipa muda wa kufanya mazoezi na kikosi kwa utulivu ili kuniwezesha kuwajua wachezaji nakuwapa mbinu zangu," amesema Robertinho.
No comments:
Post a Comment