Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa amesema hatua aliyoichukua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutengua katazo la mikutano ya hadhara inathibitisha ukomavu, uweledi, uthubutu na nia nzuri aliyonayo kwa watanzania.
Pia amesema Rais Samia anapaswa kupongezwa na kila mtanzania mpenda maendeleo bila kujali itikadi ya chama chake cha siasa kutokana na uamuzi huo aliochukua kwani ni wa Kihistoria.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi January 5, 2023, Alhaji Kimbisa alisema nia na uthubutu wa Rais Samia sio tu imekuwa nguzo muhimu ya kuchochea kasi ya maridhiano ya kisiasa nchini bali zimechangia pakubwa kuondoa mkwamo wa kisiasa ulioshuhudiwa kwa miaka sita sasa.
"CCM Mkoa wa Dodoma inaamini kuwa kuruhusiwa kwa mikutano ya hadhara kutaimarisha nguvu za kisiasa za CCM, kutapanua wigo kwa wanachama wengi zaidi kutoa mawazo chanya juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Taifa lao na kufungua fursa kwa viongozi wa Chama ngazi zote kunadi na kutangaza hadharani mazuri yote yanatekelezwa na serikali ya awamu ya sita hii ni hatua kubwa kuelekea safari ya kupata maendeleo endelevu,’’alisema.
Alisema fursa iliyotolewa na Rais Samia itatumika vizuri na itakuwa chachu ya kuzalisha mawazo bora kwaajili ya maendeleo ya taifa letu.
‘’Tuwaombe watanzania wote kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia kumuombea afya kwa Mungu,busara na maono zaidi ili aendelee kulifanyia Taifa letu mambo makubwa zaidi,’’alisema na kuongeza
‘’Ni dhahiri kuwa kwa kipindi cha miaka miwili ya uongzoi wake amefanya mambo makubwa sana hasa kwenye sekta ya miundombinu ,afya,aelimu,ulinzi na usalama, demokrasia, mahusiano ya kimataifa pamoja na uhuru wa habari,’’ alisema.
Alisema CCM mkoa wa Dodoma inamuhaidi Rais Samia na watanzania kwa ujumla kuwa tutafanya siasa za kistaarabu zisizo na lugha za maudhi, vurugu, maandamano yasiyo ya lazima ili kuonyesha ukomavu wa kisiasa kwa maslahi mapana ya nchi.
Alhaji Kimbisa alisema mikutano hiyo ya hadhara itawaimarisha katika kukosoana, kuonyeshana njia, kukumbushana juu ya wajibu na utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
January 05, 2023
Share This
About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment