HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 15, 2023

SIMBA SC YAMNASA MKATA FYUZI

Na Mwandishi Wetu

Klabu namba 12 kwa Ubora Afrika Simba SC imenasa saini ya kiungo mkabaji raia wa Burkina Faso aliyekuwa akikipiga klabu ya Diffah El Jadida ya Morocco, Hamed Ismael SAWADOGO mwenye umri wa miaka 26 na urefu wa mita 1,91.



Ni kiungo mzoefu atakae tibu shida ya ukabaji katika kiungo hasa kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika 'CAF Champions League'.

Ni aina ya mchezaji ambaye alikuwa anakosekana kwenye kikosi cha Mnyama tangu waondoke Thadeo Lwanga, Gerson Flaga, James Kotei na enzi za Patrick Mafisango.

Ni usajili unaokuja kuja kuipa Simba mamlaka ya kiulinzi na kutoa uwiano wa kuwatawala wapinzani wao katika mashindano mbalimbali.

Simba bado wako Dubai ambako leo wanamalizia kambi yao kwa kucheza mchezo wa mwisho wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi katika mji wa Abu Dhabi kuanzia majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.


No comments:

Post a Comment

Pages