HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2023

Tanzania Kuzalisha Megawatt 5000 ifikapo 2025

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limesema kuwa ifikapo Mwaka  2025 linatarajia kuzalisha Umeme hadi kufikia  Megawatt 5000 hivyo Nchi kuwa na umeme wa uhakika ambapo umeme unaozalishwa  hivi sasa ni Megawatt1300.


Hayo yameelezwa leo mbele ya Waandishi wa Habari Jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa mteja wa Shirika hilo, Martin Mwambene ambapo amesema tayari Miradi mbalimbali  ipo wanaitekeleza.

Mwambene amesema kuwa kwa sasa shirika hilo lina uwezo wa kuzalisha umeme wa megawati 1,820,wakati mitambo iliyopo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1,300 pekee.

 
 Aidha amesema tanesco  inafanya miradi kadhaa ambayo inasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka ambapo malengo ni kufikia Megawati 5000 ifikapo 2025,"amesema Mwambene

 
Hata hivyo Mwambene ameongeza kuwa TANESCO kwa kutambua matatizo ya umeme yaliyopo nchini imekuja na mradi wa Gridi Imara ambapo katika bajeti ya mwaka huu imetengewa shilingi bilioni 500 kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake.


Kaimu Mkurugenzi huyo amezungumzia pia maendeleo ya ujenzi katika Bwawa la Mwalimu Nyerere kuwa upo katika asilimia 88 na zoezi la uwekaji maji limefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari. 

 

Pia Kaimu Mkurugenzi huyo amebainisha mipango waliyonayo ya muda mfupi na mrefu wa kuzalisha umeme ikiwemo Kinyerezi na miradi mingi ya gesi, Jua, Zuzu, Singida, Shinyanga pamoja na miradi ya upepo, miradi mbadala ambayo itaongeza uwezo wa umeme.

No comments:

Post a Comment

Pages