HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 14, 2023

AFISA UTUMISHI IGUNGA AVAMIWA, AJERUHIWA KWA PANGA SHINGONI

NA MWANDISHI WETU, IGUNGA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, watu wasiojulikana wamemvamia na kumjeruhi kwa panga shingoni Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora Mussa Abdallah.


Abdallah a akiwa amejipumzisha nyumbani kwake Mtaa wa Mwayunge Kata ya Igunga mjini alipata mjasa huo baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauli ya Igunga Machi 10, 2023.

Akizungumza kwa taabu katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga ambako amelazwa kwa matibabu Afisa utumishi huyo alisema tukio hilo limetokea Machi 10, 2023 saa moja na nusu usiku.

Alisema akiwa nyumbani kwake amepumzika nje akiwa anaongea kwa simu ya mkononi  alishitukia amekatwa panga shingoni na ndipo  alikimbia kwa jirani yake ambaye ni Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga aitwaye  Lucia Kafumu kuomba msaada.

“Mimi nilikuwa nimejipumzisha nyumbani kwangu majia ya saa moja usiku baada ya kutoka katika kikao cha Baraza la madiwani lakini ghafla nilivamiwa na kukatwa panga shingoni, nyinyi angalieni nilivyokatwa kwakweli nimeonewa sana lakini Mungu namshukuru kanisaidia sikutegemea kama ntaongea hivi alisema huku akibubujikwa na machozi.

Afisa huyo alieleza kuwa huenda waharifu hao   walikuwa wamejificha kwenye shamba la mahindi lililo jaribu na nyumba yake na kwamba watu hao baada ya kumjeruhi hawakuingia ndani kuchukua kitu chochote na hata simu aliyoidondosha wakati anakimbia hawakuichukua.

Naye Mganga Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Dk Lucia Kafumu alikiri kumpokea Afisa utumishi huyo  ambapo alisema walimpokea machi 10, 2023 saa moja na nusu usiku akiwa amejeruhiwa shingoni upande wa  kushoto.

"Baada ya kufikishwa katika hospitali yetu alipatiwa huduma ya kwanza kwenye jeraha hilo na hali yake inaendelea vizuri.

Nao baadhi ya wananchi wa Igunga Mrisho Hamisi, Mariam Jumbe, Hawa Willson, Idd Jackson wameeleza kushtushwa na kitendo hicho huku wakilitaka Jeshi la Polisi kuwasaka watu hao waliofanya unyama huo.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi, Richard Abwao alithibitisha kutokea tukio hilo ambapo alisema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini mtu au watu waliohusika na tukio hilo na watakapopatikana watafikishwa mahakamani.


No comments:

Post a Comment

Pages