Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Kampuni
ya Mavazi ya Stara ya Irada Style imesherehekea miaka mitano tangu
kuanzishwa kwa Brand ya Irada Style pamoja na kusherehekea Siku ya
Wanawake Duniani.
Akizungumza na wanahabari
jijini Dar es Salaam Mmiliki wa Brand ya Irada Style, Irada Mahadhi
amesema katika kutimiza miaka mitano ya brand hiyo na kusherehekea Siku
ya Wanawake wamekuja na mavazi ya kistaarbu ya kipindi cha Mwezi wa
Ramadhan.
" Leo jioni tunashukuru siku yetu
imefika tunaitambulisha rasmi event yetu ya Fashion in Modesty ikiwa
pamoja na kuzindua Ramadhan collection yetu tusherehekea miaka mitano ya
Band ya Irada pia tunaadhimisha siku mwanamke," amesema Irada.
Amebainisha
kuwa wanasherehekea siku hiyo wakiwa na lengo la kuwasaidia wasichana
wenye vipaji wanaotaka kuingia tasnia ya mavazi ya mitindo ya
kistaarabu.
Kwa upande wake, Katibu Tawala wa
Wilaya ya Tanga, Davina Mikaya, amewapongeza Irada Style kwa kutimiza
mika mitano na kwamba wanaonyesha jinsi waliyojipanga kuwakomboa
wanawake wenye vipaji vya kufanya mavazi ya kistaarabu
No comments:
Post a Comment