March 22, 2023

Brand ya Irada Style yatimiza Miaka Mitano, yasherehekea Siku ya Wanawake yaja na Mavazi ya Stara Ramadhan


Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam

Kampuni ya Mavazi ya Stara ya Irada Style imesherehekea miaka mitano tangu kuanzishwa kwa Brand ya Irada Style pamoja na kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.


Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam Mmiliki wa Brand ya Irada Style, Irada Mahadhi amesema katika kutimiza miaka mitano ya brand hiyo na kusherehekea Siku ya Wanawake wamekuja na mavazi ya kistaarbu ya kipindi cha Mwezi wa Ramadhan.

" Leo jioni tunashukuru siku yetu imefika tunaitambulisha rasmi event yetu ya Fashion in Modesty ikiwa pamoja na kuzindua Ramadhan collection yetu tusherehekea miaka mitano ya Band ya Irada pia tunaadhimisha siku mwanamke," amesema Irada.

Amebainisha kuwa wanasherehekea siku hiyo wakiwa na lengo la kuwasaidia wasichana wenye vipaji wanaotaka kuingia tasnia ya mavazi ya mitindo ya kistaarabu.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Wilaya ya Tanga, Davina  Mikaya, amewapongeza Irada Style kwa kutimiza mika mitano na kwamba wanaonyesha jinsi waliyojipanga kuwakomboa wanawake wenye vipaji vya kufanya mavazi ya kistaarabu  


No comments:

Post a Comment

Pages