March 21, 2023

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira yakagua miradi ya Maji Shinyanga

 

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira imeanza ziara yake leo tarehe 15 Machi, 2023 katika Wilaya ya Kahama,  Mkoani Shinyanga na kukagua Miradi miwili ya Maji inayosimamiwa na Wakala wa Usambazaji Maji Vijijini (RUWASA) na Mamlaka ya Maji ya Shinyanga (SHUWASA).
 Miradi hiyo iliyokaguliwa yote inapokea maji kutoka mradi mkubwa  unaotoka Ziwa Victoria  unaosimamiwa na KASHWASA. 


Miradi hiyo miwili ni mradi wa  Kagongwa - Isaka kwenda vijiji vya Kilimbu, Jana, Butondolo na Itogwanholo.
Mradi mwingine ni mradi wa maji katika Mji wa Tinde na Shelui.

Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mheshimiwa Jackson Kiswaga (Mb) amesema Kamati imetidhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo na kuziagiza RUWASA na Mamlaka ya Maji (SHUWASA) kuangalia uwezekano wa kuongeza vituo vingine vya kuchotea maji ili wananchi wapate maji kwa ukaribu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Pages