HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 24, 2023

KIPIMO CHA JOTO LA MWILI CHATARAJIWA KUANZA KUTUMIKA KATIKA VITUO VYA MABASI NA BANDARI KAGERA


Na Lydia Lugakila, Kagera


Katika kuhakikisha hali ya udhibiti inakuwa na nguvu kubwa dhidi ya ugonjwa wa Marburg kwa ili kuzuia usisambae katika maeneo mbali mbali Mkoani Kagera, Serikali  inatarajia kuanza utaratibu wa kufanya vipimo vya joto la Mwili kwenye vituo vya Mabasi na kwenye Bandari.

Kauli hiyo imetolewa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Tumaini Nagu Machi 23, 2023 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Hospitali ya Mkoa huo.



Prof Nagu amesema katika mikusanyiko wamehakikisha uwepo wa vifaa vya kuoshea mikono mara kwa mara huku kipimo vya joto la mwili katika Stendi za Mabasi kikitarajiwa kuanza kutokana na kuwepo kwa baadhi ya wasafiri wanaoenda katika Mikoa mingine hivyo hivyo na  katika Bandari rasmi na zisizo rasmi.

Amesema kuwa hadi sasa timu ya watu 15 kutoka Wizara ya Afya  imetua Mkoani Kagera kuanzia Machi 23 hadi Machi 24 ili kuongeza nguvu ya matibabu na vifaa vya kujikinga.

Ameongeza kuwa kutokana na kasi ya udhibiti wa ugonjwa huo,visa havijaongezeka kwani wako bado wako wagonjwa 8  kati ya 5 walifariki Dunia, huku jumla ya watu 193 waliohisiwa kuwa na viashiria vya ugonjwa wa Marburg kati yao 89 ni watumishi wa Afya na 104 wako katika Jamii.

Aidha amewataka wananchi Mkoani Kagera kufika katika vituo vya afya mapema na kwa wakati, mara waonapo dalili za ikiwemo homa, Maumivu ya kichwa, kutapika, mwili kukosa nguvu na nyinginezo kama zinavyoelezwa na wataalam wa Afya nchini.

"Hadi Sasa Duniani hamna matibabu ambayo ni mahususi kwa ugonjwa huu, hivyo Wananchi jiepusheni na misiba ya washukiwa wa ugonjwa huo ,badala yake tumieni wataalam kufanya mazishi huku mkijiepusheni na uoshaji maiti pamoja na kula mizoga ya Wanyama"alisema Mganga Mkuu wa Serikali.

Hata hivyo baadhi ya Waandishi hao, akiwemo Anord Kailembo amehoji na kwa kutaka kujua hali ya wagonjwa watatu kati ya 8 waliofariki wanaendeleaje ambapo Prof Nagu amesema wanaendelea vizuri.

 

Mganga Mkuu wa Serikali amewatoa hofu wananchi mkoani humo na kusema kuwa ufuatiliaji wa karibu unaofanywa hauwezi kuruhusu ugonjwa huo kupenya kwani ugonjwa huo ni vigumu kusambaa kabla ya dalili.

No comments:

Post a Comment

Pages