Na Khadija Kalili, Kibaha
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Kibaha Mji Mhandisi Mshamu Munde ametoa ahadi ya kuongeza kiwango cha mikopo kwa wanawake na kina mama kutokana na jinsi walivyoonesha uaminifu wao katika kurudisha mikopo yao kwa wakati.
Mhandisi Munde amesema hayo leo Machi 6 katika sherehe za maadhimisho siku ya wanawake duniani iliyofanyika katika Uwanja wa Mailimoja Soko la Zamani iliyopo Kata ya Tangini Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.
"Nawaahidi kina mama wote watakao kidhi vigezo kuwa Halmashauri ya Mji Kibaha baada ya kujiridhisha na kuwakagua kwenye ziara tulizo fanya na Idara ya Maendeleo tutawaongezea kiwango cha kukopa ili muweze kupaa zaidi kiuchumi.
Munde amesema kuwa "Tumeona namna ambavyo wanawake wanavyo zalisha bidhaa mbalimbali ambazo wamezizalisha kutokana na mikopo midogo tuliyowapa awali pia nachukua fursa hiikuwapongeza wanawake kwani wanaongoza katika kufanya biashara zinazoeleweka na wameonesha mioyo ya kujituma na wanaongoza kwa kurudisha mikopo hivyo sasa umefika wakati wa kuwaongezea kiwango cha fedha za kukopa tutawakopesha kuanzia Mil.5 ,Mil.10 na kue delea" amesema Mhandisi Munde.
Akifafanua kuhusu kiwango cha fedha hizo Munde amesema kuwa Mil.400 nifedha zitakazopatikana kwenye mapato ya ndani huku Mil.300 ni fedha za marejesho ya mikopo waliyoitoa kwa kina mama wa Kibaha.
Sherehe hizo ziliambatana na shughuli za upandaji miti katika eneo la Ofisi ya Halmashaya Kibaha ambapo Katibu Tawala Kibaha Sozi Ngate ambaye alikua mgeni rasmi akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John alipanda mti wa kumbukumbu na wengine waliopanda miti ni pamoja na Mhandisi Munde , Afisa Mazingira Halmashauri ya Kibaha Ally Khatibu, Afisa Maendeleo Hamlashauri ya Kibaha Leah Lwanji.
Sherehe hizo zilipambwana wahudhuriaji wakiwemo kikosi cha Askari wanawake kutoka Kambi ya Msangani Kibaha, wajasiriamali kutoka Kibaha , wafanyakazi kutoka Idara mbalimbali za Halmashauri ya Kibaha na wakaazi wa wengine wa Kibaha.
No comments:
Post a Comment