Na Khadija Kalili
NAIBU Waziri wa Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Mheshimiwa Exaud Kigahe amewapongeza wanawake wajasiriamali na wenye viwanda nchini kutokana na namna walivyo vinara katika kujituma kujikomboa kiuchumi na kuchangia katika kukuza pato na uchumi wa nchi.
Amesema hayo katika hafla ya utoaji wa tuzo za Viwanda na Biashara iliyofanyika kwa msimu wa tatu huku ikienda sambamba kwa kutanguliwa na maonesho ya bidhaa za wanawake wenye viwanda nchini hafla hiyo ilimefanyika Machi 11 usiku kwenye Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es Salam na kuandaliwa na Chama Cha Wanawake Wafanyabiasha Tanzania (TWCC).
"Kundi la Wanawake wamekuwa wakijishughulisha katika shughuli mbalimbali za ubunifu wa bidhaa za Viwanda na kuleta tija kwa taifa na hasa ukimsaidia mwanamke kiuchumi umesaidia familia nzima" amesema Mheshimiwa Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Kigahe.
Amesema kuwa kinamama wanaongoza katika uchukuaji wa mikopo na kufanya jitihada za urejeshaji nchini kuliko makundi mengine ya wanaume na Vijana hivyo amesema serikali itaendelea kuwaweezesha kwa kuwapa mikopo kundi hilo muhimu katika jamii.
Amesema kuwa amejionea hayo alipotembelea mabanda ya wajasiriamali na wafanyabiashara kwenye viwanja vya Mlimani City na kwamba ameona bidhaa zenye ubora na viwango vinavyokidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa hivyo hana budi kuwapongeza .
"Binafsi nachukua fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwani ameifungua nchi katika sekta ya uwekezaji na kuboresha mahusiano yetu na nchi za nje kuvutia wawekezaji na kuongeza mapato ya serikali kupitia uwekezaji.
"Nawapongeza sana TWCC kwani mmeonesha ufanisi mkubwa wa kukuza uchumi wa wanawake wajasiriamali na wafanyabiashara hivyo serikali itaendelea kuthamini mchango wenu katika kukuza uchumi kwa wanawake pia nawapongeza wanawake wote nchini Tanzania kwa kujikomboa kiuchumi na kuchangia pato la taifa hivyo tunaahidi kuwa serikali itaboresha miundombinu yenu ya biashara" alisema Mheshimiwa Kigahe.
Amesema mwanamke ni nguzo imara ya familia hivyo ukimuwezesha mwanamke umefanya jambo kubwa kwenye familia serikali itaendelea kuhakikisha biashara za wanawake zinakua na zinaendelea kuleta tija kwa familia na Taifa kwa ujumla.
Mkurugenzi wa TWCC Mwajuma Hamza amesema kuwa wajasiriamali waliopatawa tuzo hizo ikawe chachu kwa wengine katika miaka ijayo.
"Tuzo hizi zikawe chachu ya kuwahamasisha na kuleta ushindani wa kibiashara ili mwakani kuwe na ushindani mkubwa"amesema Mheshimiwa Naibu Waziri huyo wa Viwanda na Biashara Kigahe.
Hafla hiyo imeandaliwa na TWCC na kudhaminiwa na Taasisi mbalimbali ambazo ni za binafsi na serikali baadhi uake ni Giz, TPSF, UN WOMAN, TGNP, CLOUDS GROUP, UMOJA WA ULAYA, AZANIA BANK,EQUITY BANK na wengineo.
No comments:
Post a Comment