Serikali
imevishauri Vyama vya Wafanyakazi na Taasisi zake kuacha kuingiza siasa
kwenye uendeshaji na utekelezaji majukumu ili kuondoa migogoro
inayoweza kujitokeza.
Hayo yamesemwa jijini Dar
es Salaam na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri (Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu) Patrobas Katambi katika Warsha ya Kuimarisha Uhusiano
Bora kati ya Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za
Fedha, Huduma na Ushauri Nchini (TUICO) na Viongozi Waandamizi wa
Taasisi zingize za Kazi.
Amesema kuwa watendaji
wa vyama hivyo kuchanganya siasa katika majukumu ya uendeshaji
kunachangia migogoro kwani vinaendeshwa kwa mujibu sheria.
"
Kuingiza siasa ndani ya vyama vya wafanyakazi kunachangia hali ya
kutoelewana nawaomba muache mfanye kazi kwa mujibu sheria nataratibu
zinazowaongoza," amesema Naibu Waziri Katambi.
Amebainisha
kuwa Serikali itaendelea kuwalinda waajiri katika kutekeleza majukumu
yao pamoja na kuwalinda wafanyakazi pale wanapodai masilaha masilahi ya
haki itendeke.
Amewaonya Mameneja Rasilimali
Watu wa Makampuni kuacha tabia ya kuwalinda waajiri kwa kwenda kinyume
na misingi ya kazi hali inayosababisha waajiriwa kukosa haki zao za
msingi ikiwemo kuondolewa kazini kiholela.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa TUICO, Boniface Nkakatisi amesema warsha
hiyo ina lengo la kukuza uhusiano kati ya chama hicho na taasisi zingine
za kazi.
Amefafanua kuwa katika warsha hiyo
mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo majukumu ya vyama vya wafanayakazi
pamoja na umuhimu wa mikataba ya pamoja katika kuimarisha uhusiano
sehemu za kazi.
Nae, Afisa Mtendaji Mkuu wa
Chama cha Waajiri Nchini (ATE), Suzanne Ndomba amesema cha hicho
kitaendelea kushirikiana na TUICO na taasisi zingine pamoja kuhakikisha
waajiri wanawapa fursa wafanyakazi kujiunga na vyama hvyo.
Mwenyekiti
wa TUICO, Paul Sengeze amesema chama hicho kinatambua umuhimu wa
uhusiano na vyama vingize vya kazi na kusisitiza kuwa vyama vya
wafanyakazi sio adui wa waajiri bali kinafanya kazi kutetea haki na
masilahi ya pande zote.
Rais wa Shirikisho la
Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya ameipongeza
TUICO kwa kuonyesha ushirikiano na vyama vingine huku akiongeza Sikukuu
ya Wafanyakazi itafanyika Mkoani Morogoro Mei Mosi Mwaka huu.
Jaji
Mfawidhi- Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Jaji Yose
Mlyambina amesema bado kuna migogoro mingi ya kazi huku idadi ya majaji
ikiwa ndogo hivyo ipo haja ya kuwepo tume shsirikishi yenye jukumu la
kutoa elimu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
Shirika Kazi Duniani Nchini Tanzania (ILO) Bw. Maridadi amesema ILO
itaendelea kutoa mafunzo kwa TUICO ili kuimarisma uhusiano borao kati ya
chama hicho na taasisi zingine.
No comments:
Post a Comment