Na Hussein Ndubikile, Dar es Salaam
Taasisi
ya Foundation For Disabilities Hope (FDH) imetoa msaada wa mafuta ya
ngozi kwa wanafunzi Wenye Ulemavu wa Ngozi huku ikibainisha kumuunga
mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake anazozifanya za
kusaidia watu wenye ulemavu na shughuli za miradi ya maendeleo.
Akizungumza
katika hafla ya utoaji wa msaada iliyofanyika katika Viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Michael Salali
amesema kuwa wamekuwa wakijihusisha katika utoaji misaada kwa makundi
maalum na kwamba anaamini mafuta hayo yatawasaidia wanafunzi kuwakinga
na mionzi ya jua.
" Tumeshatoa misaada kwa
makundi ya watu wenye ulemavu tunatoa mafuta haya kuwasaidia wanafunzi
wenye ulemavu wa ngozi hatutaishia hapa tutaendelea kuwasaidia tunaomba
wadau watuunge mkono," amesema Salali.
Amebainisha
kuwa kabla ya kutoa msaada huo tayari walishatoa Bima kwa Watu 1,000 na
vifaa vingine vya kuwasaidia watu wenye ulemavu hivyo wataendelea
kushirikiana na Serikali kusaidia makundi maalum.
Akimpongeza
Rais Dkt. Samia amesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi
amefanya mambo ikiwemo kuboresha miundo ya afya, elimu na usafirishaji
na kwamba ameonesha kuwajali walemavu.
Kwa
upande wake, Naibu Spika ambaye pia na Mbunge wa Jimbo la Ilala (CCM),
Mussa Azzan Zungu ameishukuru taasisi hiyo kwa msaada iliyoutoa kwa
wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi na kuziomba taasisi zingine kuiga
mfano.
Nae, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ameipongeza FDH kwa jinsi
inavyowajali watoto wenye ulemavu na kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.
Samia.
Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam Mwalimu Beatrice Edward ameipongeza taasisi hiyo
inavyojitoa kusaidia wanafunzi wenye ulemavu huku akiziomba taasisi
kujitokeza kusaidia watoto wenye mahitaji maalum.
No comments:
Post a Comment