March 28, 2023

TAKUKURU PWANI YAMULIKA UDANGANYIFU VYAMA VYA USHIRIKA VYA MSINGI VYA MAZAO NA MASOKO (AMCOS)

Na Khadija Kalili


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana  Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani  leo asubuhi Machi 28 wametoa  taarifa  kwa kipindi cha robo ya Oktoba  hadi Desemba  mwaka 2022 ambayo imebaini madudu na udanganyifu  kwenye Vyama  vya Ushirika  na Vyama vya Msingi  vya Mazao  na Masoko (AMCOS).



Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Pwani Christopher  Myava amesema kuwa TAKUKURU wamefanya  kazi ya ufuatiliaji wa miradi 75 ya maendeleo  yenye thamani  ya Mil.11,421,038,710.71 katika sekta  ya Elimu, Afya, Maji na Barabara ambapo wamebaini kuna upungufu mchache  kwenye utekelezaji ikiwa ni pamoja na  Shule ya  Sekondari  Viziwaziwa  iliyopo Wilayani Kibaha  Mjini wenye thamani ya  Mil.470 (470,000,000)  mabati yaliyotumika kuezekea jengo la Utawala  Maabara,  na Vyoo vya Shule. Hayakuwa  na kiwango  kilichothibitishwa  kuezekea  majengo ya serikali ambayo  ni geji 28 badala yake  yalitumika  mabati ya geji 30.


"TAKUKURU tumeanza kufanya uchunguzi  na hatua kali za kisheria  zitachukuliwa kwa wote  waliohusika  baada ya uchunguzi kukamilika" amesema Kamanda Myava.


Kamanda  Myava amesema kuwa  ukarabati wa Skimu  ya  maji Kijiji cha Mkongo Wilayani Rufiji yenye thamani Mil.500 (512,208,249.03), imebainika katika tanki moja  la kuhifadhia  maji  linavujisha pia milango ya  jengo la Ofisi ya Jumuia  ya watumiaji maji Kijiji TAKUKURU na Ofisi ya Meneja  wa Mamlaka ya Usambazaji  maji  vijijini (RUWASA)tumekubaliana  kuwa RUWASA wahakikishe  mkandarasi anarekebisha  mapungufu yaliyobainika  kabla ya muda wa matazamio kuisha" amesema Kamanda Myava.


Akizungumzia kuhusu uchambuzi wa mifumo amesema kuwa  ili kudhibiti mianya ya rushwa  katika Idara za Serikali na sekta  binafsi  chambuzi za mifumo tatu zimefanyika  kwenye maeneo  ya  uendeshaji  na usimamizi  wa masoko ya biashara pamona  utekelezaji  miradi kwa kutumia 'force account' katika Vyama vya Ushirika vya msingi vya  mazao  na masoko (AMCOS)  vya Mkongo  Kilimani ,Kitupa, Nyaminywili, Kipo na Ngorongo AMCOS  zote za Wilayani Rufiji Mkoani Pwani.


Amesema  kuwa katika uchambuzi huo wamebaini  kuwepo kwa  udhaifu katika utunzaji  wa nyaraka  na kumbukumbu za Vyama vya Ushirika ambapo  baadhi ya nyaraka  zimekuwa  zikitunzwa  nyumbani kwa viongozi wa bodi  huku akiitaja  AMCOS ya Kipo kuwa baadhii ya nyaraka zake  zimeonekaba kuharibiwa na mchwa.


"Hatua hii ya kukosa kumbukumbu  ya nyaraka  zilizoharibika imesababisha changamoto  katika kubaini mapato na matumizi ,takwimu na taarifa zote  za fedha  kwa ujumla" amesema Kamanda huyo.


Aidha ameweka wazi kuwa maazimio  yaliyowekwa  ni kuwa ujenzi  wa Ofisi bora ya kutunza  nyaraka na kumbukumbu za Ushirika uwe umekamolika ifikapo mwaka  2024.


Kuandaa  taarifa za fedha na  kujaza taarifa  sahihi  katika  nyaraka zote  za Ushirika na kuhakikisha zinatunzwa vizuri ikiwa ni pamoja na kununua bomba la kupulizia  dawa za wadudu waharibifu.


"TAKUKURU tumebaini kuwa  upo udanganyifu  wa kutoandika  idadi ya kilo sahihi kulingana  na mzigo  wa mkulima  wakati wa upimaji kwa kisingizio  cha ubora  na unyaufu, mfano.mwananchi anafika na kilo 30.5 lakini kwa makusudi  ya kufanya  udanganyifu wapimaji  ambao ni wajumbe  wa Bodi  ya AMCOS  husika wanamwambia mkulima mazao yako  hayana ubora hivyo badala ya kilo 30.5 tutakuandikia kilo 29." 


Hali hii ikiendelea  kwa  wakulima  zaidi wajumbe  hao  watajikusanyia  kilo nyingi kwa udanganyifu  nakutengeneza  mauzo  kwa majina  hewa  kwa manufaa yao, wananchi wanapogundua udanganyifu huu huacha  kuuza  mazao  kwenye AMCOS zao  na kwenda  kuuza AMCOS za Kata  jirani  jambo ambalo AMCOS mama zinakosa  mapato lakini  pia wananchi wanalazimika  kutafuta huduma hii.


" TAKUKURU tumechukua  hatua za kuwataka  kuongeza matumizi ya mizani ya kidigitali na kupunguza matumizi ya mizani ya kusogeza ,pia mazao yenye ubora  yasichanganywe ili wakulima wapate madaraja  stahiki" amesema Kamanda  Myava.


Ameongeza kwa kusema kuwa wametoa maelekezo ya kuandaliwe  daftari rasmi  la mapokezi ambalo  wajumbe  wa Bodi  watakuwa wakilihakiki na kusaini kila tarehe ya mapokezo ya mazao.


Imebainika kuwa  AMCOS ya  Mkongo ya Rufiji  kutotoa stakabadhi  kwa wakulima  mara  baada ya kupokea mzigo  baadaye wakulima  hupewa stakabadhi zilizoandikwa kiasi  cha kilo  yofauti na kile  kilichoandikwa awali  wakati  wa kupokea  mzigo  hali hii hutengeneza mianya ya rushwa kwa hao  wajumbe wa bodi  wasio  waaminifu wanaopima mazao  kutoka kwenye kilo zile  walizowapunja  wakulima na kutengeneza  mauzo kwa faida  yao hivyo kusababisha hasara  kwa Ushirika na wakulima.


"Tumebaini kuwa matumizi ya skabadhi  za kuandika na mkono  badala ya POS kukusanyia  ushuru ambazo pia wakati  mwingine hazitolewi  baada ya  malipo kufanywa mfano soko kuu la Mji wa Utete, soko la Kijiji Ikwiriri ukusanyaji wa mapato  bila kutoa skakabadhi  ya mashine POS kwa kisingizio  cha ubovu  wa mashine  hali inayosababisha  upotevu  wa mapato yanayokusanywa ikiwemo soko la Mnarani Wilayani Kibaha  wafanyabiashara waliohojiwa baadhi wamedai kutopatiwa  skakabadhi za malipo kutoka kwa wakusanya ushuru.


Hivyo basi  tumeagiza  kuongeza ufanisi wa matumizi ya POS katika kukusanya ushuru ili kuongeza mapato,ikiwemo kufanha  ukaguzi  wa mara  kwa mara  ili kuongez usimamizi kwa wakusanya  ushuru kwa lengo la kudhibiti.ukusanyaji mapato.


Mwisho Kamanda Myava ametoa wito  wa TAKUKURU kwa wananchi  na wadau wote katika Taasisi za serikali  nansekta binafsi  kuunga  mkono  program  ya TAKUKURU RAFIKI kwani inahusisha  jitihada  za kutambua  na kutatua kero zinazoweza kusababisha  uwepo  wa vitendo  vya rushwa  kama zitaachwa bila kushughulikiwa kwenye sekta  za maji, elimu, nishati (Umeme), afya, barabara, ardhi, huduma za jamii na miradi ya maendeleo inayotekelezwa ba serikali, utatuzi wa kero zitakazoibuliwa kupitia programu hii unatarajjwa kuimarisha  utoaji huduma ,kuboresha utekelezaji wa miradi  ya maendeleo ,kuimarisha uzingatiaji wa misingi ya Utawala Bora na kupunguza vitendo vya rushwa

No comments:

Post a Comment

Pages