Na John Richard Marwa
Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kuvunja mkataba na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu yao ya Wanawake Yanga Princess Sebastian Nkoma kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Yanga wamemfikia hatua hiyo mara baada ya kikosi chao cha Yanga Princess kukosa matokeo katika michezo mitatu mtawalia ambayo pia Nkoma hakuwa sehemu ya benchi la Ufundi, Walipoteza dhidi ya Fountain Gate Princess, wakatoka sare dhidi ya Mkwawa Queens pamoja na sare dhidi ya Simba Queens.
Nkoma anaicha Yanga Princess nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Soka la Wanawake Serengeti Lite Women's Premier League (SWPL) ikizidiwa pointi tano na watani zao Simba ambao wako nafasi ya tatu huku wakizidiwa pointi saba dhidi ya vinara Fountain Gate Princess.
Duru zinaeleza kumekuwa nankutokuwa na maelewano kati ya Kocha Nkoma na Uongozi kutokana na kila upande kuwa na mtazamo tofauti juu ya kikosi hicho, Nkoma anaamini timu inahitaji muda kuunganika Ili kuweza kushindania ubingwa huku Uongozi ukiamini timu inapaswa kushindania ubingwa msimu huu.
Nkoma anaungana na Edna Lema ambaye alianza na kikosi hicho kama Kocha Mkuu msimu huu kabla ya kutimuliwa baada ya michezo miwili ya kwanza ya msimu ambapo Yanga Princess walifungua msimu kwa kupoteza dhidi ya Fountain Gate Princess na mchezo wa pili wakashinda mabao manne kwa mtungi dhidi ya Mkwawa Queens.
Kocha Nkoma ni miongoni mwa makocha ambao wamepata mafanikio katika Soka la Wanawake. Msimu uliopita alitwaa ubingwa wa SWPL akiwa na Simba Queens kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Mganda Charles Lukula kwenye Fainal za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Soka la Wanawake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Uongozi kupitia mitandao ya Klabu imeeleza kuwa kwa Sasa timu itakuwa chini ya Kocha Fedy Mbuna hadi mwisho mwa msimu huu.
No comments:
Post a Comment