March 12, 2023

TASAC YAKANUSHA MALALAMIKO YA VIJANA ZAIDI YA 400 WALIOVUNJIWA MIKATABA BILA UTARATIBU

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

MKURUGENZI Mkuu wa TASAC Kaimu  Mkeyenge amekanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko dhidi ya Shirika hilo ikiwemo Mikataba ya mafunzo kazi kwa vijana zaidi ya 400 waliokuwa TASAC ilivunjwa bila kufuata utaratibu huku ikiwa imebaki muda wa mwaka mmoja kuisha kwa mikataba hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi huyo wakati akitoa ufafanuzi kwa Umma kuhusu Vijana waliokuwa wanafanya shughuli za Mafunzo ya kazi ndani ya shirika hilo.

"Mkeyenge amesema kuwa tuhuma walizotoa Vijana hoa kuwa wanafanya kazi bila bima ya afya na kwamba TASAC ilitoa rushwa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) katika mashauri ya kazi yaliyofunguliwa na vijana hao ili haki isitendeke,"

 "Hakuna  sheria inayomtaka muajiri yeyote yule kumkatia bima ya afya kijana anayefanya shughuli za Mafunzo kazini suala hilo halipo na hakuna taasisi yeyote inayoweza kufanya hivyo kwani stahiki zao zimeainishwa kwenye Muongozo wa Kitaifa wa Mafunzo Kazi uliotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu na tuhuma kuhusu TASAC kutoa rushwa kwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ili mashauri ya kazi yaliyofunguliwa na vijana hao haki isitendeke hakuna ukweli wowote''amesema Mkeyenge

Aidha Mkeyenge amesema vijana 209 waliofutiwa mikataba yao, ni vijana 41 tu ambao hawakuridhika na maamuzi hayo ambapo vijana 32 kati ya vijana 41, shauri lao lilifutwa na CMA kwa kuwa liliwasilishwa nje ya muda, hivyo ni vijana 9 tu ambao shauri lao dhidi ya TASAC lilipokelewa na lipo katika Tume ya Usuluhisi na Uamuzi.

Ambapo vijana 168 waliobaki hawakupinga uamuzi wa TASAC wa kuvunja mikataba yao kutokana na mabadiliko ya Sheria ambayo yalikuwa ni nje ya uwezo wa Shirika.

Mkurugenzi huyo amesema suala hilo lipo kwenye chombo cha maamuzi kisheria, TASAC haipaswi kuzungumzia shauri hilo ila waliona ni busara kulitolea ufafanuzi wa kilichofanyika kwa upande wa TASAC na kuacha hatua za maamuzi zinazoendelea kuchukua mkondo wake.

"TASAC ni Shirika la Umma linalotekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo inayotolewa na Serikali, hivyo linatoa wito kwa Umma kuwa na subira wakati Tume inapoyafanyia kazi mashauri hayo," amesema

Katika hatua nyingine amesema TASAC ni taasisi ya Serikali inayosimamiwa na Sheria, Kanuni na Miongozo ya Serikali, hivyo basi mashauri yake kisheria yanasimamiwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ikiwa ni pamoja na shauri hili hivyo kwa mantiki hiyo, Shirika hilo halijatoa na haiwezi kutoa rushwa yoyote kwa CMA ili kuzuia haki isitendeke kama ilivyoripotiwa katika mitandao ya kijamii.

''Kwa mantiki hiyo, niwahakikishie kuwa TASAC haijatoa na haiwezi kutoa rushwa yoyote kwa CMA ili kuzuia haki isitendeke kama ilivyoripotiwa katika mitandao ya kijamii'' amesema  Mkeyenge

Hata hivyo Mkeyenge amehitimisha kwa kusema kati ya vijana 209 waliofutiwa mikataba yao, ni vijana 41 tu ambao hawakuridhika na maamuzi hayo Vijana 32 kati ya vijana 41, shauri lao lilifutwa na CMA kwa kuwa liliwasilishwa nje ya muda, hivyo ni vijana 9 tu ambao shauri lao dhidi ya TASAC lilipokelewa na lipo katika Tume ya Usuluhisi na Uamuzi.

No comments:

Post a Comment

Pages