March 12, 2023

WAZIRI BITEKO AMTAKA KATIBU MKUU KUSIMAMIA MALENGO

Na Jasmine Shamwepu, Dodoma

WAZIRI wa Madini Dotto Biteko amemtaka Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Kheri Muhimbali kusimamia malengo ambayo wizara hiyo imekabidhiwa na serikali kuyafanyia kazi ili yakamilike kwa wakati.

Alisema katika wizara hiyo wapo watu wa aina mbalimbali ambao katibu mkuu atakwenda kufanya nao kazi hivyo anapaswa kuwa makini ili kuhakikisha kazi zinafanyika na kufikia malengo ya serikali kama ambavyo yamepangwa.

Waziri Biteko, ameyasema hayo leo jijini hapo,katika kikao cha kumtambulisha katibu mkuu hoyo, kwa watumishi wa idara zote za wizara ya madini.

Amesema Katika wizara hiyo wapo watu wa kila aina wapo ambao ukiwapa kazi wao wanaangalia ‘dead line’ hata kama kazi uliwapa haijakamilika wanakuletea, lakini wapo ambao kazi hawamalizi kwa wakati na wala majibu hawawasilishi.

"Lakini pia wapo ambao wao kazi hawafanyi kabisa, lakini wapo wengine ambao wao ukiwapa kazi wanafanya na ukiwarekebisha wanafurahi kurekebishwa lakini wengine ukiwarekebisha wanakukasilikia"alisema Biteko

"Kutokana na muda mwingi watumishi kuutumia wakiwa kazini katibu mkuu anatakiwa kuwafanya waajiriwa kujiona wao ni wa muhimu katika wizara hiyo.

Naye Naibu waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa, amesema yapo mambo mengi ambayo wameyafanyia kazi hadi sasa ikiwemo kupunguza idadi ya watu waliokuwa wamekaimu katika nafasi mbalimbali ndani ya wizara hiyo.

"Katibu mkuu nashukuru kuwa umeeleza kuwa unapaenda kufanya kazi kama timu mie pia ni muumini wa ushirikishwaji lakini tangu nimeingia madarakani katika nafasi hii ni mwaka mmoja na miezi kadhaa mambo mengi tumeyafanyia kazi ikiwemo kupunguza idadi ya watu walikua wakikaimu katika nafasi mbalimbali.

Hata hivyo ameomba katika nafasi ambazo bado hazijafanyiwa kazi uone ni namna gani zinafanyiwa kazi ili maeneo yanayokaimiwa yapate watu na kazi ziendele kwa malengo tulijiwekea.


No comments:

Post a Comment

Pages