HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 15, 2023

SEKTA YA ELIMU YAASWA KUFUNGUA MIPAKA AFRIKA MASHARIKI

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf  Mkenda, akifungua kongamano la wadau wa sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika masuala ya elimu jijini Dar es Salaam leo Machi 15, 2023 ambapo washiriki kutoka nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki komgamano hilo.

 

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akizungumza wakati wa mkutano wa 12 Academia-Public-Private Partnership Forum (APPPF) uliofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 15-17, 2023

Katibu Mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki (TUCEA), Prof. Gaspard Banyankimbona, akizungumza wakati wa Mkutano wa 12 wa Academia-Public-Private Partnership Foruma (APPPF).  

Mkurugenzi wa Sekta za Jamii Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Irene Isaka, wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau wa sekta ya umma na sekta binafsi katika masuala ya elimu ambapo nchi saba za Jumuiya ya Afrika Mashariki zimeshiriki pamoja na nchi ambazo si wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mwakilishi kutoka Serikali ya Ujerumani ambaye pia ni Mkuu wa Ushirikiano wa Kikanda katika Balozi wa Ujerumani, Johannes Fechter akitoa mada katika kongamano hilo.
Baadhi ya washiriki.
Picha ya pamoja.




Na Costancia Nkindi

Wana Taaluma sekta ya Elimu wameaswa kufungua mipaka ya Elimu na Ajira ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda akifungua Jukwaa la 12 la Wana Taaluma sekta ya Umma na Sekta Binafsi linalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia leo.

Waziri Mkenda amesema ili kufanikisha hilo yanahitajika majadiliano ya mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kupitia mawaziri wa Elimu husika Ili nchi zote kuwa na mlengo mmoja.

"Ili kufanikisha hilo tunahitaji sekta zetu na mawaziri wa Elimu tupate fursa ya kukaa pamoja chini ya Baraza la Vyuo Vikuu Afrika Mashariki tuone tunaweza kufanya nini.

"Lakini vile vile tunahitaji kushirikisha sekta binafsi ambazo zitaweza kutoa msaada kwa wanafunzi kwa mifano mikopo ambayo mwanafunzi ndani ya jumuiya naweza kunifaika nayo akitoka nchi moja kwenda nyingine ndani ya jumuiya yetu. " Amesema Waziri Mkenda

Kwa upande wa Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Charles Kihampa amesema lengo la jukwaa ni kuwakutanisha  Wana Taaluma sekta ya Umma na Sekta binafsi katika mashirikiano na kuangalia namna ya kukuza mashirikiano mbalimbali hasa katika kuleta tija ya Elimu inayotolewa na Taasisi za Elimu ya juu.

" Wamealikwa wenye viwanda wako hapa, wamekuwepo pia waajiri pia wako wa sekta binafsi na kuna maonesho ya mbalimbali.

"Kwahiyo unapokuwa na wadau kama hawa wanakuwa na fursa ya kujadili na kuona wapi pakufanyiwa maboresho Ili kuendana na mahitaji ya mitaala na sera za Elimu lakini pia kutoa wataalamu wenye ubora unaohitajika kwenye Taasisi zao." amesema Prof. Charles Kihampa

Nae Dk. Irene Isaka amesema kongamano hilo litasaidia kuondoa mwanya uliopo kati ya wahitimu wa Vyuo Vikuu na Vyuo mbalimbali na fursa mbalimbali za ajira.

"Kama jumuiya ya Afrika Mashariki tunatoa Sera na miongozo mbalimbali ambayo inawezesha wanafunzi wetu waweze kujairika. Sio hiyo tu pamoja na kuweza kufanya kazi nchi nyingine ndani ya jumuiya yetu ya Afrika Mashariki.

"Unaweza ukawa mtanzania ukapata ajira nchi nyingine ndani ya jumuiya na wataalamu kutoka mataifa wanachama kuajirika nchi nyingine zote ndani ya jumuiya yetu.

Kongamano hilo limeshirikisha nchi Saba wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania, Rwanda, Uganda, Kenya Burundi, Dr Kongo pamoja na nchi shiriki za Zambia, Zimbabwe na Ethiopia.

No comments:

Post a Comment

Pages