Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi (WAMM), Rahma Kassim Ali (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini "B" Hamid Seif Said wakiwa katika eneo la Mgogoro wa Ardhi Fujoni, Unguja.
Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Rahma Kassim
Ali ameuagiza uongozi wa Kamisheni ya Ardhi Zanzibar kushirikiana na
ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Magharibi "B" kuirudisha serikalini eka
iliopo fujoni kufuatia kutumika kinyume na utaratibu.
Eka hiyo inayomilikiwa na Faki Rashed Faki lakini anadaiwa kuikata
viwanja na kuviuza kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kinyume na matumizi ya
shughuli za kilimo yaliyowekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mhe. Rahma ametoa
agizo hilo alipofanya ziara kuitembelea eneo hilo mara baada ya kupata
taarifa kutoka kwa mwananchi kuhusiana na uuzwaji wa eneo hilo la eka ya
serikali.
"Hatua ya kurudisha serikalini eka hii itakua ni
funzo kwa wale wote ambao walipewa eka kwa ajili kuziendeleza kwa
shughuli za kilimo na badala yake kuzitumia eka hizo kwa kuzikata
viwanja na kuuza"Alisisitiza waziri Rahma.
Ameongeza
kuwa Wizara ya Ardhi Zanzibar itahakikisha inazifatilia kwa makini eka
zote za Serikali na yoyote atakaegundulikana anakwenda kinyume na
matumizi sahihi ya eka hizo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi
yake.
Hata hivyo Waziri
Rahma amewataka wananchi wanapotaka kununua maeneo kufika Kamisheni ya
Ardhi Zanzibar kwani Taasisi hiyo imeundwa kisheria katika kusimamia
masuala yote yanahusiana na ardhi na umiliki wa Ardhi.
Waziri Rahma alifafanua kuwa hatua hiyo itasaidia
kueupusha migogoro ya ardhi Zanzibar inayoweza kuepukika endapo wananchi
watafuata sheria.
Aidha
waziri rahma alisisitiza mwananchi yoyote aliyepewa eka na anataka
kubadilisha matumizi ya ardhi afuate taratibu zikizowekwa.
Naomba
niwaeleza wananchi wanaomiliki ekari za Serikali, Wizara ya Ardhi
imeweka utaratibu maalum wa kuwasilisha mabadiliko ya matumizi ya ardhi
kwa kamisheni ya Ardhi na Wizara iwapo yatakwenda sambamba na mpango
wa Serikali haitokuwa na pingamizi maamuzi hayo" alisema waziri rahma
Kwa
upande wake mkuu wa Wilaya ya Kaskazini " B" Hamidi Seif Said ameahidi
kulitekekeza agizo hilo kwa vitendo na amesema wilaya hiyo haitosita
kumchukulia hatua mtu yoyote atakaekwenda kinyume na maagizo ya
Serikali katika matumizi ya ekari hizo kwa maslahi ya nchi na taifa kwa
ujumla.
Nae ndugu Faki
Rashed Faki ambae anadai kuwa eka hiyo amerithi kutoka kwa mzazi wake na
amekata viwanja kwa kuuza kwa watu wawili tofauti amedai kuwa
alikua hajui kama eka za Serikali hazitakiwi kuuzwa na kufanya hivyo ni
kosa kisheria.
Katika
hatua nyengine Waziri Rahma. alipata nafasi ya kumtembelea Mzee Hafidh
Ali Mdachi huko Bumbwisudi alielitoa eneo lake kupisha Mradi wa ujenzi
wa hospital ya Wilaya huko jang'ombe kwa binti hamran na kuagiza
kamisheni ya ardhi kutafutia ufumbuzi tatizo la eneo alilopewa fidia
kuwa tayari limeshaendelezwa.
No comments:
Post a Comment