HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 12, 2023

KADA WA CCM SINGIDA ATOA FUTARI VIJIJI VITATU KWA WENYE UHITAJI


Mjumbe  wa Kamati ya Utekelezaji kupitia Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM  Mkoa wa Singida, Ahmed Misanga, ambaye pia ni Katibu wa Taasisi ya Faraja Foundation (kulia) akimkabidhi Imam wa Msikiti wa Sepuka,Juma Mohamed Mughenyi boksi lenye tende kwa ajili ya futari kwa waislam wenye uhitaji wa Misikiti mitatu ya vijiji vya Mwaru, Sepuka na Irisya vilivyopo Wilaya ya Ikungi mkoani hapa kwa ajili ya Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

 

Na Dotto Mwaibale, Singida

 

 WAKATI Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ukielekea kumalizika na kubakiza siku kumi Mjumbe  wa Kamati ya Utekelezaji kupitia Jumuiya ya Wazazi na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi ( UVCCM) na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM  Mkoa wa Singida, Ahmed Misanga, ambaye pia ni Katibu wa Taasisi ya Faraja Foundation ametoa futari kwa waislam wa vijiji vitatu vilivyopo Wilaya ya Ikungi mkoani hapa.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi futari hiyo iliyofanyika Aprili 11, 2023 Kata ya Sepuka, Misanga alisema ametoa futari hiyo pamoja na tende kwa ajili ya waislam wenye uhitaji kutoka vijiji hivyo katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ambapo kufunga ni nguzo ya nne ndani ya  dini hiyo.

“Sadaka hii niliyoitoa imewalenga zaidi waislam wenye uhitaji, mayatima, wajane, wazee na wengine wote kwani dini yetu ndivyo inavyoelekeza tuwajali wenzetu wa makundi hayo” alisema Misanga.

Misanga alisema sadaka hiyo ameitoa kwa misikiti mitatu ya vijiji vya Mwaru, Sepuka na Irisya  na kuwa inatolewa kupitia Tasisi ya Faraja Foundatio ambapo ni muendelezo wa utoaji futari katika Mkoa wa Singida.

Akizungumza wakati akipokea sadaka hiyo kwa niaba ya misikiti hiyo mitatu, Imamu wa Msikiti wa Kata ya Sepuka, Juma Mohamed Mghenyi alimshukuru Misanga kwa kutoa futari hiyo ambayo imewalenga waislam hasa wenye uhitaji katika kipindi hiki cha mwisho wa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mughenyi alisema waislam wengi wamekuwa na changamoto mbalimbali ambapo alitumia nafasi hiyo kuwaomba waislam na watu wengine kuwa na moyo wa huruma na kuiga jambo hilo alilolifanya Misanga kupitia Taasisi ya Faraja Foundation kujitoa kwa vitu mbalimbaliili kusaidia watu hao wenye uhitaji.

”Jambo alilolifanya Misanga ni jambo kubwa sana na hapa kwetu halijawahi kutokea wito wangu kwa waislam leteni nguo, viatu, baibui, kanzu na vitu vingine vinavyo fanana na hivyo ili tukavitoe kwa wenzetu hao wenye uhitaji” alisema Mughenyi.

Sadaka hiyo ilipokelewa na viongozi kutoka vijiji hivyo ambao ni Omari Mgisa, Imamu wa Msikiti wa Kata ya Mwaru, Jumanne Kungu, Kata ya Irisya na Jumanne Mughenyi (Sepuka)

Wazee wa Kislam wa Kata ya Sepuka wakimshukuru, Misanga, kwa futari hiyo.

 Misanga akikabidhi futari hiyo (Tende) 

No comments:

Post a Comment

Pages