Na Victor Masangu, Kibaha
Katika
kuchagiza chachu ya kuleta maendeleo kwa wananchi mfuko wa Jimbo
kutoka ofisi ya Mbunge wa Kibaha mjini imeamua kutoa zaidi ya kiasi cha
shilingi milioni 20 katika kusaidia kuinua na kuchochea kasi ya
maendeleo katika sekta mbali mbali.
Hayo
yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvesty Koka wakati
wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuweza kukagua na kutembelea
baadhi ya miradi ambayo inatekelezwa kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.
Ziara
hiyo ambayo iliambatana na wajumbe mbali mbali wa mfuko wa Jimbo pamoja
na viongozi wengine wa Chama Cha mapinduzi (CCM) ngazi za
matawi,mashina,kata,pamoja na wilaya ili kuweza kujiridhisha kama miradi
hiyo inafanyika kwa kiwango kinachotakiwa
Akizungumza
pindi alipokuwa katika miradi hiyo Koka alisema kwamba katika fedha
hizo ambazo zilishatolewa ni kwa ajili ya kuchochea zaidi kasi ya
maendeleo katika miradi mbali mbali ikiwemo,afya,elimu,miundombinu ya
barabara maji na huduma nyingine za kijamii.
Aidha
Mbunge huyo alifafanua kwamba katika fedha hizo zimeweza kusaidia mambo
mbali mbali ikiwemo ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi na
sekondari,ununuzi wa madawati na viti katika shule mpya ya sekondari
Misugusugu.
Pia
aliongeza kuwa katika fedha hizo zimeweza kutumika katika kuanzisha
mradi wa ujenzi wa wodi ya mama na mtoto katika kata ya Mbwawa kwa lengo
la kuwasaidia wakinamama wajawazito kuondokana na changamoto ya
kutwmbea umbari mrefu kufuata huduma ya kujifungulia.
Sambamba
na hilo alifafanua kuwa dhamira yake kubwa ni kuwaletea wananchi
maendeleo kwa pamoja na hususan atazipa kipaumbele kwa Hali na mali kata
ambazo zipo pembezoni mwa mji.
"Mimi
Kama Mbunge lazima niweke mipango madhubuti ya kushirikiana na wananchi
na ndio maana nimeamua kutumia fedha hizi za mfuko wa Jimbo ili
kuchochea kasi ya maendeleo na mieanza ziara yangu katika kata zipatazo
sita na nitamalizia na nyingine kwani Jimbo langu lina kata 14,"alisema
Koka.
Nao baadhi ya
wananchi ambao wamenufaika miradi hiyo ambayo imetokana na fedha za
mfuko wa Jimbo wameishukuru serikali ya awamu ya sita pamoja na Mbunge
Koka kwa kujikita zaidi katika kuwaletea maendeleo yenye tija kwa
maslahi ya jamii kwa ujumla.
Fedha
za mfuko wa jimbo zimekuwa zikitolewa kwa ajili ya kuweza kuchochea
maendeleo kupitia miradi mbali mbali ikiwemo afya,elimu,maji,umeme, miundombinu ya barabara,pamoja na huduma nyingine za kijamii.
Ziara
hiyo ya Mbunge wa Jimbo a Kibaha mjini ya kutembelea miradi yamaendeleo
imefanyikakatika kata sita ikiwemo Mbwawa, Visiga, Misugusugu, Viziwaziwa, Kibaha, pamoja na kata ya mkuza.
Mbunge wa Jimbo la
Kibaha Mjini akiwa na viongozi wa CCM pamoja na wajumbe wa mfuko wa
Jimbo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment