Na Khadija Kalili
MTANGAZAJI maarufu wa Kituo Cha Redio kongwe nchini Clouds FM Mwemba Burton almaarufu kama Mwijaku ametangazwa kuwa Mwenyekiti wa Chawa wa Mama Mkoa wa Dar es Salaam .
Katibu wa Chawa wa Mama Taifa Neema Karume amesema kuwa uteuzi huo umekuja baada ya Mwijaku kukidhi vigezo vya kuwa na nguvu ya uhamasishaji katika masuala ya Chama na Serikali na jamii nzima kwa ujumla.
Uteuzi huo umefanyika Aprili Mosi mwaka 2023 Jijini Dar es Salaam .
"Tunamkaribisha sana ili tuungane kwa pamoja kuyasema yale yote mazuri anayoyafanya Rais wetu mpendwa Dkt.Samia Suluhu Hassan hakika mama amefanya makubwa hatuna budi kumuunga mkono katika juhudi zake zote" amesema Katibu wa Chawa wa mama Taifa Neema Karume.
Katibu huyo wa Chawa Taifa Neema ameongeza kwa kusema kuwa kundi la Chawa wa Mama linaundwa na watu kutoka kada mbakimbali nchi nzima huku akiyataja baadhi yao makundi hayo kuwa ni Madereva wa Bodaboda , Madereva Taxi, Mabasi ya Abiria, Mama Lishe ,Wakulima, Wafugaji,Wafanyabiashara wakubwa na Wamachinga, Wasusi, Wavuvi, Wanasiasa, Wanafunzi wa Vyuo, Waalimu, Wakurugenzi katika taasisi mbalimbali Wafanyakazi wa Serikali na Taasisi binafsi na Watanzani waliopo nje ya nchi ( DIASPORA).
Neema amesema kuwa lengo la kundi la Chawa wa Mama ni kuhakikisha wanakuwa Mabalozi wazuri ndani na nje ya nchi kwakuyasemea yake mazuri yanayotekelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuhakikisha ifikapo mwaka 2025 wanaweka historia kwa Rais Dkt. Samia Hassan kuliongoza taifa katika awamu ya saba.
Amesema kuwa Mwijaku amechaguliwa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Jiji la Dar es Salaam Diwani wa Viti Maalumu Beatrice Nyamisago ambaye pia ni Afisa Habari Chawa wa Mama Taifa kuamua kuachia nafasi hiyo .
"Nyamisago ameona si vema kushikilia nafasi mbili hivyo ameomba ang'atuke katika nafasi ya Mwenyekiti wa Dar Es Salaam" amesema Neema.
No comments:
Post a Comment