HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 01, 2023

RT YAANIKA KIKOSI CHA U 20 & 18 MASHINDANO YA AFRIKA LUSAKA ZAMBIA


NA TULLO CHAMBO, RT


SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), limetangaza wanariadha 15 kuunda timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 na 18 itakayoiwakilisha nchi katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika jijini Lusaka, Zambia Aprili 29 hadi Mei 3 mwaka huu.

Kikosi hicho kimetangazwa na Makamu wa Rais wa RT, William Kallaghe, mara baada ya kumalizika mashindano maalumu ya majaribio kwa ajili ya kupata timu itakayoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo.

Mashindano hayo, yalifanyika leo Aprili Mosi, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, ambako jopo la makocha chini ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Alfredo Shahanga na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Ufundi, walifanikisha zoezi hilo.

Akitangaza majina ya wateule hao, Makamu wa Rais wa RT, Kallaghe, alilipongeza jopo hilo la wataalamu sambamba na chama mwenyeji (DAA), kwa kufanikisha jukumu hilo nyeti kwa Taifa.

Kallaghe, aliipongeza mikoa na wanariadha binafsi waliojitokeza kwenye zoezi la leo, na kwamba hata wale ambao hawajateuliwa kuingia timu ya Taifa, wasikate tamaa, bali wazidishe juhudi kwani rekodi zao tayari zimeingia kwenye mfumo wa shirikisho.

Makamu huyo wa Rais, aliwataka wachezaji na viongozi waliopewa dhamana katika timu huyo, kuweka mbele nidhamu katika kila jambo mbele yao, kwani ndio msingi wa mafanikio.

"Timu hii inaanza kambi leo hii hii bila kuchelewa chini ya Makocha Alfredo Shahanga na Bi. Asha Abdallah Khatib kutoka Zanzibar, kambi itakuwa pale hosteli za Baraza la Maaskofu, nawaomba sana mzingatie nidhamu kwani ndio kila kitu...Itakaa hapo hadi tutakapoanza safari ya Zambia, na tunaishukuru Serikali kwa kutuwezesha usafiri Wa basi, hivyo tutatoka hapa taratibu tutapumzika Mbeya, then kesho yake tunaingia Lusaka," alisema Kallaghe.

Timu iliyoteuliwa ni kama ifuatavyo:

No comments:

Post a Comment

Pages