HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 25, 2023

UJUMBE KUTOKA ANGOLA WATUA NCHINI KUJIFUNZA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA TASAF

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Angola ambao wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya namna Mfuko wa Maendeleo ya Jamii – TASAF unavyotekeleza majukumu yake kupitia Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bw. Ladislaus Mwamanga akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha Maafisa wa Serikali kutoka Angola ambao wako nchini kujifunza utekelezaji wa shughuli za TASAF

Mkurugenzi Msaidizi FAS Bi. Rosa Teixeira de Carvalho (katikati) akizungumza kwenye kikao cha kuukaribisha Ujumbe huo ikiwa ni mwanzo wa ziara ya kujifunza shughuli za TASAF zinavyotekelezwa. Kiongozi wa Shughuli za FAS katika Benki ya Dunia Bw. Boban Paul akitoa maelezo ya utangulizi wakiwa katika ziara ya mafunzo ya namna Mpango wa Kunusuru Kaya za Walengwa unavyotekelezwa

Meneja wa Mipango na Utafiti wa Taasisi ya Mfuko wa Fidia kwa Mfanyakazi (WCF) Bw. Patrick Ngwila akiwasilisha mada kuhusu maandalizi na maendeleo ya sera ya taifa ya hifadhi ya jamii kwa Maafisa wa Serikali kutoka Angola ambao wako nchini kujifunza utekelezaji wa shughuli za TASAF

....................................

Ujumbe wa maafisa kutoka Angola uko nchini kwa ziara ya mafunzo kuhusu utekelezaji wa shughuli za TASAF. Ujumbe huo ukiongozwa na kiongozi wa shughuli za mradi huo katika Benki ya Dunia Bw. Boban Paul umefuatana pia na Mkurugenzi Msaidizi wa FAS Bi. Rosa Teixeira de Carvalho wameishukuru TASAF Serikali ya Tanzania kwa kutoa kibali kwa ujumbe huo kutembelea TASAF kwa nia ya kujifunza. Ujumbe huo wa watu kumi utakuwepo nchini kwa muda wa siku tano.

Akiwakaribisha wageni hao kwenye Ofisi ya TASAF Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Mwamanga aliwahakikishia wageni hao kuwa watajifunza mambo mengi kutoka TASAF inayotekeleza Mpango wa Kunusuru kaya za walengwa ambao una lengo la kuwapatia wananchi maisha bora. Wageni hao watapata nafasi pia ya kutembelea walengwa katika Halmashauri za Wilaya za Kibaha na Bagamoyo.

Wageni hao walipata mawasilisho kuhusu Utekelezaji wa TASAF ambayo mpaka sasa umeshaandikisha kaya za walengwa zaidi ya milioni moja na laki tatu. Kaya hizo za walengwa hupata ruzuku na kufanya kazi za ajira ya muda na kujiunga kwenye vikundi vya kuweka akiba na kufanya shughuli za ujasiriamali.

Kati ya masuala ambayo ujumbe huo umepata nafasi ya kujifunza katika siku ya kwanza ya ziara hiyo ni namna TASAF inavyofuatilia utekelezaji na kuhakikisha kuwa walengwa wanapata stahiki zao kwa wakati, taratibu za utekelezaji wa miradi ya miundo mbinu na taratibu za utambuzi wa walengwa.

Ujumbe huo pia utafanya mawasilisho kuhusu Mradi wa KWENDA ambao unatekelezwa nchini Angola kwa utaratibu kama wa TASAF na hivyo kutoa nafasi ya TASAF na ujumbe huo kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa miradi.

No comments:

Post a Comment

Pages