Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bwakira Chini wakiwa katika mkutano na Wadau wa elimu pamoja na Mashirika wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET). |
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akizungumza katika mkutano na wanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Msingi Bwakira Chini, walipofanya ziara shuleni hapo. |
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga akizungumza na wanafunzi wa kidato cha pili Shule ya Msingi Bwakira Chini, walipofanya ziara shuleni hapo. |
WADAU wa Elimu pamoja na Mashirika wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) wamefanya ziara katika baadhi ya shule za msingi na sekondari zilizopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro DC ikiwa ni sehemu ya shughuli za maadhimisho ya Juma la elimu kwa Mwaka 2023 yanayofanyika Kitaifa Wilaya ya Morogoro DC, mkoani Morogoro.
Shule zilizotembelewa na wadau hao wa elimu ni pamoja na Shule ya Msingi Njia Nne, Shule za Msingi Bonye na Duthumi, na Shule ya Sekondari Bwakira ambapo imefanyika Mikutano ya uhamasishaji wa Jamii wakiwemo Wanafunzi, wazazi na walimu kushirikiana katika kutatua changamoto anuai za elimu katika maeneo hayo.
Aidha akizungumza katika mikutano hiyo, Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga ameitaka jamii hiyo kuona umuhimu wa kuchangia uboreshaji wa elimu.
Aliongeza kuwa shughuli za maadhimisho ya juma la elimu zinalenga kuhamasisha na kukumbusha jamii, serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau mbalimbali wa elimu kuona umuhimu wa uchangiaji wa elimu kwa kuzingatia kauli mbiu ya mwaka huu; isemayo “Tuboreshe uwekezaji wa rasilimali za ndani kwenye elimu kwa maendeleo Endelevu.
Mashirika ya Mtandao wa Elimu Tanzania yanayo shiriki katika kongamano hilo linaloendelea Kata ya Mvuha mkoani Morogoro ni pamoja na; KCBRP, TECDEN, BOC, KESUDE, AWPD, SMD, Beyond Giving, St. Justine Centre, LSSF, EOTAS, Sengerema, CDH, NELICO, CBIDO, MDREO, CBR Rulenge, SARDIVA na Disability Relief.
Mashirika mengine ni LVDC, TEN/MET Secretariat, UWEZO Tanzania, Hakielimu, Plan International, KCBRP, BRAC, World Vision, We world, Milele Zanzibar, CAMFED, Right to Play, Room to Read, UNICEF na Feed the Children.
Maadhimisho ya Juma la Elimu (Global Action Week for Education (GAWE) 2023 ambayo yalifunguliwa rasmi Aprili, 17 yanatarajiwa kufikia tamati kesho kutwa Aprili, 21, 2023.
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bw. Ochola Wayoga () akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Njia Nne walipofanya ziara shuleni hapo. |
No comments:
Post a Comment