Mkurugenzi Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Wellworth, Zulfikar Ismail,
akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu shughuli zao,
katikati ni Ofisa Sheria na Utawala Saimon Nguka na pembeni ni Ofisa
Masoko Mwandamizi wa Wellworth Josephine Makundi.
Na Selemani Msuya
KAMPUNI
ya Wellworth inayojihusisha na uwezekezaji katika sekta ya hoteli za
kitalii nchini imeeleza kusikitishwa na tuhumu za kuwa wameshindwa
kuendeleza Hoteli ya Embassy, Kunduchi Beach na Mikumi Lodge kwa miaka
14.
Kauli hiyo ya
kusikitishwa imetolewa na Ofisa Sheria na Utawala wa Wellworth, Saimon
Nguka, wakati akijibu tuhuma zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa
wa Katavi Taska Mbogo, alizozitoa Februari mosi Bungeni jijini Dodoma.
Nguka
ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam, amesema kampuni yao imesikitishwa na taarifa walizodai ni za
uongo zilizotolewa na mbunge huyo na kutoa rai kwa wabunge na viongozi
wengine wa umma kutafuta taarifa sahihi kabla hawajatoka hadharani
kuzungumza.
“Februari
mosi Mbunge wa Viti Maalum, Taska Mbogo alitolea mfano hoteli zetu za
Embassy, Kunduchi Beach na Mikumi Lodge, kwamba tangu zibinafsishwe ni
takribani miaka 14 sasa, lakini hakuna shuguli inayoendelea.
Aliendelea
kudai kiwa ndani kila kitu kimeharibika na kwamba mwekezaji aliyepewa
hoteli hizo ni mmoja, hivyo amevunja mkataba wa ubinafsishaji na haoni
sababu ya Serikali kuendelea kumbembeleza, bali aandikiwe barua ya kuja
mezani kwa maridhiano,” alinukuu maneno ya Mbunge.
Ofisa
huyo alisema taarifa hiyo ambayo ametoa mbunge huyo Februari mosi
ilikuwa ya uongo na wao kama kampuni wameandika barua mara mbili
kumueleza Spika kuwa mbuge huyo amepotosha umma na kumueleza ukweli
ulivyo, ila hawajapata majibu, hivyo wamelazimika kujitokeza na kuelezea
hali halisi.
Nguka
amesema Kampuni ya Wellworth haijatelekeza hoteli yoyote na taarifa kuwa
wamekaa miaka 14 bila kuendeleza ni uongo wa mchana kweupo akitolea
mfano kuwa Januari 6, 2018 ndio walipata barua ya kibali namba
NaTNP/HQ/P.30/17 cha ujenzi wa Mikumi Wildlife Lodge.
Lakini wameingia mkataba Januari 30,2021 na sio kama anavyodai Mbunge Mbogo.
“Tunapenda
kuwajulisha kwamba pamoja na zoezi la kusaini mkataba miaka miwili
iliyopita, ila shughuli za ukarabati zinaendelea, baada ya kukamilisha
taratibu zote za kisheria na matarajio yao ni mapema mwaka 2024 tutaanza
kutoa huduma na kuajiri zaidi ya watanzania 96,” amesema.
Akifafanua
kuhusu Hoteli ya Embassy, Nguka amesema Kampuni ya Wellworth imenunua
jengo kutoka kwa Kampuni ya Enterprise Tanzania Limited na sio kwamba
imebinafsishiwa kama alivyodai mbunge huyo na kwamba kuchelewa kwa
ujenzi kunatokana na kesi ambazo zipo mahakamani.
“Tulinunua
jengo hilo kutoka kwa muuzaji na sio Serikali kwa utaratibu wa biashara
ya kawaida, ila kuna kesi zimefunguliwa makamani, hivyo zikiisha
tutaendelea na uwekezaji kwani tulishakamilisha michoro ya ujenzi ili
Embassy Hoteli iwe ya nyota tano.
Tulikamilisha
taratibu za kupata mkopo wenye thamani ya dola za Marekani milioni 23
kutoka mabenki mbalimbali, ili kujenga jengo lenye ghorofa 13, hivyo nia
ya kuendeleza ipo, tunadhani mbunge hakuwa na taarifa sahihi,” amesema.
Aidha,
Nguka amesema Hoteli ya Kunduchi Beach kwa sasa wanaendelea na
ukarabati ili iwe na hadhi ya nyota tano ambapo ikikamilika itakuwa
inasimamiwa na kampuni kubwa ya uendeshaji wa hoteli za kimataifa.
Ofisa
huyo amesema hoteli hiyo ikikamilika itaweza kutoa ajira za moja kwa
moja kwa watu zaidi 220, hivyo kuwezesha Wellworth kuajiri zaidi ya watu
800.
Amesema ukarabati wa Kunduchi Beach umechelewa kutokana na urasimu wa utoaji kibali unaofanywa na baadhi ya maofisa wa Serikali.
“Bila
msaada wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na Ofisi ya Msajili wa
Hazina, hadi sasa kungekuwa hakuna ukarabati, ila kwa sasa kazi
inaendelea kama anavyotaka Rais Samia Suluhu Hassan na matarajio yetu
2024 huduma zitaanza kutolewa,” amesema.
Naye
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Wellworth, Josephine Makundi amesema kampuni
hiyo kwa sasa inamiliki hoteli 22 ambazo zinaweza kulaza watu zaidi
1,000 kwa siku.
Makundi
amesema iwapo biashara ya hoteli hasa za kitalii itaendelea kuimarika
wataweza kutoa ajira kwa watanzania wengi na kuchangia pato la taifa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Wellworth,
Zulfikar Ismail amesema wamejipanga kuongeza uwekezaji ili kuunga mkono
juhudi za Rais Samia katika kukuza uchumi.
“Sisi
tunaataka siku chache zijazo tuwe kampuni ya wazawa ambayo inaongoza
katika sekta ya hoteli nchini, na hili linawezekana kwani kwa sasa tuna
hoteli 22 ambazo zina uwezo wa kuchangia zaidi Sh.bilioni 6 kwenye pato
la taifa kwa mwaka, tunaomba wasaidizi wa Rais wasiwe kikwazo,” amesema.
Ismail
amesema hadi sasa wamewekeza zaidi ya dola milioni 200 za Marekani
ambazo ni takribani bilioni 500, hivyo wamedhamiria kuipaisha sekta hiyo
kwa kujenga mahoteli ya kisasa ambayo yatavutia watalii kote duniani.
No comments:
Post a Comment