HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 16, 2023

Airtel yazindua kauli mbiu mpya, Sasa ni Á Reason to Imagine’ kauli mbiu mpya kuendana na wateja wote

Mkurugenzi Mtendaji Airtel Tanzania Dinesh Balsingh (wakwanza kulia) akiwa na Wakurugenzi wengine wa kampuni hiyo wakionyesha mabango maalum ikiwa ni ishara ya kuzindua kauli mbiu mpya ya Airtel ‘Reason to Imagine’. Kauli mbiu hiyo ya ‘Reason to Imagine’ inalenga kujenga uhusiano kwa Vijana na kuwawezesha wateja wake kufikia kila fursa.

 

 Na Mwandishi Wetu

 

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Afrika ambayo inaongoza kwa huduma bora za mawasiliano na huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi na ambayo inafanya biashara kwenye nchi 14 barani Afrika, leo imezindua kauli mbiu mpya  ‘A Reason to Imagine’ inayolenga kujenga ujumuishi wateja wa rika zote wakiwemo  Vijana na wateja wake wote Afrika.

Akiongea leo Kuhusu kauli mbiu mpya Á Reason to Imagine’ Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Dinesh Balsingn alisema  Airtel Baada ya Airtel kutamba na kauli mbio ya The Smartphone Network sasa tunakuja na A Reason to Image ambapo lengo letu ni Kuendeleza dhamira yetu ya kuwawezesha wateja wa rika zote wakiwemo vijana kufikia ndoto au matarajio yao.

Bw, Balsingn alieleza “Kila mtu anayo sababu  ya kufanikiwa kupitia maono, vipaji, watu wanaomzunguka na fursa alizonazo. Sisi Airtel Kupitia mtandao wetu uliosambaa kote tumejipanga kukuwezesha kufikia malengo yako kupitia watu na fursa zilizokuzunguka, vipaji vyako kwenye chochote kama vile kuimba, kucheza, kuandaa video na hata kuigiza. Ni kwa huduma zetu bora kama Data, Airtel Money au kupiga simu, sms unazotumia ukiwa popote.

Kwa maana hiyo, kampeni hii inalenga kusherehekea kujitoa, ubunifu na uvumbuzi wa Vijana wa Afrika, na Tanzania ambapo asilimi 60 ya watu wake wana umri chini ya miaka 25. Kwa wateja wetu hapa Tanzania na masoko mengine, fikra chanya ni muhimu sana na kwa kufanya mambo yaende vizuri, ishi kulingana na nyakati. Tunawasaidia Vijana wetu kufikiria upya nafasi zao kwa kutumia mtandao wetu kuungana na familia, marafiki, biashara na kubadilisha kila hali kuwa fursa. Tupo kwa ajili ya kufanya mawazo yatimie…tupo hapa kufungua fursa’ alisema Balsingh.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Biashara Airtel Afrika Anthony Shiner alisema ‘Vijana ni muhimu katika kuiendeleza Afrika. Zaidi ya asilimia 60 ya watu Barani Afrika wako chini ya miaka 25 na kwa kuwezesha kizazi hiki ni kufanya Mapinduzi makubwa kwa mustakabali wa baadae wa Afrika.

‘Kwa kupitia kampeni na kauli mbiu yetu hii, A Reason to Imagine tunathibitisha dhamira ya Airtel ya kuendeleza maendeleo ya Vijana wa Afrika kwa kubadilisha kila nafasi  kuwa fursa’ alisema Shiner. 

 Kampeni ya ‘Reason to Imagine’ ni kampeni kubwa zaidi kwa Airtel Afrika. Inajumuisha mfululizo wa matangazo ya runinga na mchanganyiko wa machapisho maalum kwenye kila sehemu tunayofanya biashara kwa lengo la kuendeleza ubunifu  mtandaoni, na kwenye mabango kwa njia ya simu za mkononi.

Udhamini wa sasa wa The Voice of Afrika ni mfano halisi wa jinsi Airtel Afrika inavyowapa Vijana sababu ya kuonyesha uwezo wao, kwa kushirikiana na The Voice kuleta kipindi hiki. The Voice Afrika inaonyesha vipaji vya kipekee vya muziki wa kiafrika katika onyesho ambalo pia linashirikisha jopo  la waalimu wa mziki na watangazaji wa TV. Kati ya washiriki 100 waliochanguliwa kuingia fainali, kijana mmoja wao ataweza kuwa mshindi katika kipindi ambacho kinarushwa moja kwa moja kwenye vituo vya TV bila malipo katika bara zima na pia kwenye Airtel TV. Hii ni moja ya mipango ambayo Airtel Africa imewekeza katika kukuza vipaji vya vijana na utaalamu katika elimu, michezo, na sekta ya ubunifu.

No comments:

Post a Comment

Pages