HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 18, 2023

DC KYERWA APIGA MARUFUKU WATOTO KUFUNGIWA CHAKULA KIPORO

 


Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Zaitun Msofe akizungumza katika kikao Cha baraza la madiwani.


Na Lydia Lugakila, Kyerwa.


Mkuu wa Wilaya ya  Kyerwa Mkoani Kagera, Zaitun Msofe amepiga marufuku tabia ya baadhi ya Wazazi, kuwapa Watoto Chakula kiporo maarufu Pamba ili waende nacho na wakitumie shuleni Kama mlo.


Msofe ametoa kauli hiyo kupitia kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika Wilayani humo alipopata nafasi kutoa  maelekezo ya Serikali.


Amesema ni wakati sasa kupiga vita kwa hali na mali tabia hiyo kwani wapo wataalam wamepita na kuona kwamba mtoto anachukua kiporo cha chakula kilichopikwa tangu usiku ambacho mtoto ukitunza na kwenda nacho shuleni.


"Mtoto anashinda na Chakula kilichopikwa Jana usiku anakaa nacho kuanzia asubuhi hadi mchana anapoenda kukila kinatoa povu kimeishaharibika ebu tuwahudumie watoto tuseme Pamba basi" alisema Mkuu huyo wa Wilaya.


Amesema ni wakati sasa kwa wazazi kufuata mwongozo wa Serikali wa kuwachangia chakula shuleni watoto wao ili. wapate lishe bora.


Ameongeza kuwa lishe katika Wilaya ya Kyerwa haiko vizuri kwani Wananchi wamezoea kutumia chakula kimoja ambacho ni ndizi.


Amewasisitiza Madiwani Wilayani humo kuhakikisha wanaendelea kutoa Elimu kwa Wananchi ili wazingatie mlo kamili wasitumie ndizi  tu kama chakula peke yake.


Aidha amelipongeza Baraza la Halmashauri la wilaya hiyo kutokana na ushirikiano mzuri ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Bahati Henerco kwa niaba ya madiwani hao ameahidi kuyatekeleza vyema maelekezo ya Serikali huku akimpongeza Rais Dokta Samia kwa kuendelee kuijenga Kyerwa katika sekta mbali mbali ikiwemo ya afya Elimu.


Hata hivyo amewaomba madiwani hao kuweka jitihada zaidi kudhibiti Magendo ya Kahawa.

No comments:

Post a Comment

Pages