Na Victor Masangu, Kibaha
Katika
kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kukuza na
kuinua mchezo wa netiboli mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Selina
Koka ametoa vifaa mbali mbali vya mchezo huo kwa wanawake wa kata ya
Mbwawa ili waweze kuanzisha timu ya mchezo huo.
Mke
wa Mbunge huyo ambaye pia ni mlezi wa Jumuiya ya umoja wa wanawake
(UWT) Wilaya ya Kibaha mji ametoa vifaa hivyo wakati wa ziara la
Mwenyekiti Uwt katika kata ya Mbwawa yenye lengo la kuzungumza na
wanachama pamoja na kukiimarisha chama.
Selina
alisema anatambua Kuna wanawake wengi wenye vipaji ndio maana akaamua
kutoa sapoti ya kuchangia vifaa hivyo kwa ajili ya kukuza mchezo wa
netiboli hususan kwa wanawake wa Jimbo la Kibaha.
"Natambua
kwamba tupo katika ziara hii ya UWT lakini mm katika kuendeleza sekta
ya michezo nimeona ni vizuri kutoa vifaa hivi kwa wanawake wa ccm kata
ya CCM ili wawze kuonyesha vipaji vyao katika mchezo wa
netiboli,"alisema Selina.
Alisema
kwamba amepania kuanzisha ligi ya mpira wa kikapu katika kata mbali
mbali na kwa kuanzia ametoa jezi 14 pamoja mpira kwa ajili ya kuanzisha
timu ya mchezo wa netiboli kwa wanawake wa kata ya Mbwawa.
Katika
hatua nyingine alitoa wito kwa wanawake wanafanya mazoezi na kuanzisha
timu za mpira wa netiboli na kuahidi kuendelea kushirikiana nao bega kwa
bega katika kuukuza mchezo huo.
Kwa
upende wake Mwenyekiti wa Juimuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Elina
Mgonja alimpongeza Selina Koka kwa kuona umuhimu wa kukuza mchezo wa
netiboli pamoja na kutoa vifaa vya michezo kwa wanawake hao.
Nao
baadhi ya wanawake wa chama cha mapinduzi ambao wamepatiwa vifaa hivyo
vya michezo wameahidi kuvitunza pamoja na kuunda timu ya kata ya mchezo
wa netiboli ili kuweza kulete mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika
mchezo huo.
No comments:
Post a Comment