NA STEPHANO MANGO, NAMTUMBO
KAMPUNI ya Mantra Tanzania inayomiliki Mradi wa Urani wa Mto Mkuju, wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma imetoa katika msimu wa 2022/2023, Kampuni imeweza kusaidia vikundi sita kutoka vijiji vya Likuyu, Likuyu Mandela na Mtonya kwa kuwapa pembejeo za kilimo na kuwa na Mashamba darasa katika kilimo cha mahindi, alizeti na mpunga.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya Mantra Tanzania, Khadija Kawawa akizungumza hivi karibuni na Waandishi wa Habari katika Kata ya Likuyuseka alisema kuwa katika kukabiliana na changamoto ya ajira katika kata ya Likuyuseka ambapo vijana wengi wanataka waajiriwe na Mantra katika mradi wake wa Urani, kampuni imeonelea ni vema kuwawezesha wanaLikuyu kuweza kujikwamua kiuchumi katika shughuli ya kiuchumi ambayo wanaiweza na kuifahamu vema ambayo ni kilimo.
Kawawa alisema kuwa pembejeo hizo zenye thamani ya Shs milioni ishirini na mbili ni pamoja na mbegu, madawa na mbolea, ambapo kati ya vikundi hivyo vya wakulima kimoja wapo ni kikundi kilichoundwa na Kaya maskini za Kijiji cha Likuyu.
Aidha katika hatua nyingine Kampuni hiyo imetoa miche mia tano ya matunda aina mbalimbali ikiwemo Miparachichi kwa kikundi cha Mwamko na shule zilizopo kata ya Likuyuseka ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji wa kampuni hiyo kwa jamii iliyokaribu nayo.
Akikabidhi miche hiyo Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Khadija Kawawa alisema kuwa miche hiyo ni miparachichi, michungwa, miembe na mipapai yenye jumla ya thamani ya Sh.1,800,000 (Milioni moja na laki nane).
Kawawa amesema kuwa ni matarajio ya Mantra kuwa miti hiyo itatoa chachu kwa Kata ya Likuyuseka kupanda miti ya matunda ambayo itaboresha lishe kwa wakazi hao na kuwaongezea kipato.
Kawawa amesema kuwa matunda yatakayozalishwa na kikundi cha Mwamko ambacho ni mnufaika wa msaada huo wa miti ya matunda, yatauziwa kampuni ili yatumike kama sehemu ya lishe kwa wafanyakazi na vibarua wakaokuwa wanafanya kazi katika Mradi wa Urani.
Akizungumzia kuhusu miche hiyo afisa uhisiano huyo amesema Miche hiyo pia imetolewa kwenye shule ya sekondari ya Selous iliyopo Kijiji cha Likuyu na Shule ya Sekondari Mary Wilson iliyopo Kijiji cha Likuyu Mandela, huku malengo ya kutoa miche ya matunda kwenye shule hizo ili kusaidia kuboresha afya za wanafunzi kwa kupata milo kamili wawapo shuleni.
Kawawa amesema kuwa ni matarajio ya kampuni kuwa matunda yatakayozalishwa na kikundi cha Mwamko ambacho ni mnufaika wa msaada huo wa miti ya matunda, yatauziwa kampuni ili yatumike kama sehemu ya lishe kwa wafanyakazi na vibarua wakaokuwa wanafanya kazi katika Mradi wa Urani.
Kwa upande wake katibu wa kikundi cha Mwamko Rajabu Kombo akipokea miche hiyo amesema kuwa wanaishukuru kampuni ya Mantra kwa msaada huo ambao ni mwendelezo wa msaada ulioanza kutolewa tangu mwaka 2021 ambako umewawezesha kuanzisha kitalu cha miti ambayo wamekuwa wakiiuza kwa mashirika mbalimabali ikiwemo Mantra, Vyama vya Ushirika na watu binafsi.
Kombo amesema kuwa Miche hiyo ya matunda itakuwa mkombozi kwa wanakikundi kwa vile itawaongezea kipato na kuboresha afya za familia zao na kuwa watatumia mafunzo na uzoefu watakayoyapata kuwafundisha wenzao kuhusu kilimo cha kisasa cha mbogamboga na matunda.
Amesema kuwa matarajio ya kikundi kuwa mradi wa Mantra utakapoanza kufanya kazi ya uchimbaji wanakikundi hao watakuwa ndio wauzaji wakubwa wa mbogamboga na matunda kwenye Kampuni hiyo na kisha kujipatia vipato.
Naye Mtawa (Sista) Celeste ambaye ni mkuu wa shule ya Mary Wilson ameishukuru Kampuni ya Mantra kwa msaada huo ambao utaboresha afya za wanafunzi na kuwapatia kipato kwa kuuza ziada itakayopatikana.
Mkuu huyo amesema kuwa shule ya Wasichana ya Mary Wilson wameazimia kuhakikisha hakuna mche wa mtunda utakaokufa kwa kuwa watatumia mfumo wa kumkabidhi kila mwanafunzi mche wake na itakuwa ni mashindano kuona nani anautunza vizuri mche wake.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Selous ambayo ni shule ya Kata ya Likuyuseka, ameihakikishia kampuni ya Mantra kuwa miche hiyo itatunzwa kwa weledi na ustadi mkubwa ili kuhakikisha inapona yote licha ya kuwepo kwa changamoto ya Wanyama wa porini watadhibitiwa kwa tutengeneza uzio.
No comments:
Post a Comment