HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 08, 2023

RC CHALAMILA AONYA WAKANDARASI MIRADI YA MAJI KAGERA

 Na Lydia Lugakila Kagera


Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Arbert John Chalamila, ameshuhudia utiaji saini mikataba 13 ya maji, yenye thamani ya shilingi Bilioni 7.57 inayojengwa katika Wilaya za Mkoa huo, huku akiwaonya Wakandarasi kutogeuka chanzo cha kukwamisha miradi hiyo.

Akishuhudia utiaji saini mikataba hiyo Chalamila aliwapongeza Wakandarasi hao walioaminiwa Kama sehemu ya utekelezaji wa Miradi  ya maji huku akiamini uhaba wa maji Mkoani humo kwenda kufikia mwisho.


"Niwaombe nyinyi mlioaminiwa mkatekeleze miradi hiyo kwa ufanisi mkubwa, sitegemei kuona mnakwamisha Miradi hiyo na kusababisha kuonekana ya Mwisho kuweni makini sitaki kumdondosha Rais Samia kwani kawekeza fedha nyingi katika Miradi hiyo" alisema RC Chalamila.


Aidha amewasihi kutotaka kupata faida kubwa, jambo linalowafanya Wakandarasi wengi kutokamilisha miradi kwa wakati.


Amewasisitiza pia kuepuke kuweka vijana wasio na anuani maalum wanaoweza kujihusisha na tabia ya wizi katika Miradi hiyo mikubwa ya Serikali.


Naye Meneja Ruwasa Mkoa wa Kagera Mhandisi Walioba Sanya ameishukuru Serikali na kuomba kuendelea kuwaamini  Wakandarasi hao ili watekeleze Miradi hiyo kwa kiwango ambapo wanataraji Miradi hiyo ikamilike mwezi Desemba 2023.


Hata hivyo naye mmoja wa Wakandarasi kutoka Wilaya ya Karagwe Oscar Pastory amewashukuru viongozi Mkoani humo kwa kuwaamini ambapo ameahidi kutowaangusha kwani atatekeleza majukumu hayo kwa kiwango Bora.

No comments:

Post a Comment

Pages