Mratibu wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida, Shabani Mukee (kushoto) akizungumza na viongozi wa taasisi hiyo kutoka wilaya zote za Mkoa wa Singida, katika kikao kazi kilichofanyika May 13, 2023. Kulia ni Mhasibu wa taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Hadija Misanga.
........................................................
Na Dotto Mwaibale, Singida
TAASISI ya isiyoya Kiserikali ya Sisi Tanzania Mkoa wa Singida imewakutanisha viongozi wote wa
taasisi hiyo kutoka wilaya zote saba za Mkoa wa Singida, katika kikao kazi chenye lengo la kujadili masuala yao
pamoja na kampeni kadhaa walizozipanga kuzifanya.
Akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika May 13, 2023 Mratibu wa
taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Shabani Mukee alisema baadhi ya kampeni hizo ni
kuwatembelea wahitaji waliopo kwenye makundi maalum kama wajane, wagane na yatima kwa ajili ya kufanya
hisani kwa kutoa misaada ya kijamii.
Alisema walengwa wengine wa kampeni hiyo ni wanafunzi ambao wapo pembezoni
ambao kwa namna moja ama nyingine wanashindwa kwenda shuleni kutokana na
changamoto mbalimbali.
"Sisi Tanzania Mkoa wa Singida tumejipanga kuwafikia watoto wenye
changamoto hizo wakiwemo waliopo katika mazingira magumu na kuhakikisha
mahitaji yao yanatimizwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyotusaidia," alisema
Mukee.
Mukee alisema ajenda nyingine
walioijadili ni suala zima la kuwaandaa vijana kuja kuwa viongozi hivyo
wanatarajia kuendesha semina kwa vijana wa Mkoa wa Singida na anaamini baada ya
mwaka mmoja watapatikana vijana wengi ambao watakuwa viongozi katika kada
mbalimbali na baadhi yao kujitokeza katika chaguzi za mbeleni kugombea nafasi
za uongozi.
Alitaja mkakati mwingine kuwa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kupanda mti kwenye kila kwaya ambao utaitwa mti wa mkuu wa kaya ambao utapandwa katika kila nyumba iliyopo Mkoa wa Singida ili kuufanya mkoa mzima kuwa ni wa kijani.
Alisema taasisi hiyo inaamini kampeni hiyo ikifanikiwa itaisaidia serikali
katika kukabiliana na tabia nchi kwa kuhifadhi mazingira.
Alisema viongozi walioudhuria kikao hicho walitoka wilaya ya Mkalama,
Iramba, Manyoni, Itigi, Ikungi, Singida DC na Manispaa ya Singida.
Katibu Mkuu Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Singida, Emmanuel Digha
alisema vijana wana umuhimu wa kujiunga na taasisi hiyo inawaunganisha kwa
pamoja kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowahusu na kuzitafutia ufumbuzi.
"Umuhimu wa vijana kujiunga na Sisi Tanzania itatusaidia vijana
kupeana fursa mbalimbali na kuelezana changamoto zinazo tukumba na hatimaye
tuweze kulijenda taifa katika nyanja za kiuchumi, kijamii na kisiasa,"
alisema Digha.
Naye Hellen Pascal ambaye ni Mratibu wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Singida
alisema Sisi Tanzania mkoani Singida inawaunganisha vijana wote waliopo katika
vyuo mbalimbali vya Serikali, watu binafsi na taasisi za dini.
Alisema wanawakutanisha vijana ili wazielewa fursa zilizopo ndani ya
taasisi hiyo kutokana na vijana wengi kutozifahamu ili wazijue na kuzitumia
waweze kutoka kimaisha.
Mjumbe wa taasisi hiyo Gwau Msafiri alisema kazi nzuri ya kutoa hisani kwa
makundi yenye uhitaji inayofanywa na Sisi Tanzania ni ya muhimu kwa jamii
ambapo alitoa ushauri kuwafikia na
walengwa ambao hawafikiwi kutokana na kuishi maeneo ya pembezoni.
" Mara nyingine watu wenye mahitaji ambao ufikiwa ni wale ambao wapo
kwenye miji na shauri twende mbele zaidi kwa kuwafikia waliopo pembezoni mwa
miji ambako kuna watu wenye changamoto nyingi ukilinganisha na wale waliopo
kwenye maeneo ya mijini," alisema Msafiri.
Mratibu wa taasisi hiyo Wilaya ya Singida Mjini Masanja Sitta alisema wao wamejikita kutembelea
vyuoni na mashuleni kuhamasisha wanafunzi kuzingatia maadili na kupinga vitendo
vyote vya ukatili wa kijinsia na kutojiingiza katika ndoa za jinsia moja na
usagaji.
Afisa Miradi wa taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Abdallah Shabani alisema
kutokana na changamoto kubwa ya ajira kwa vijana tumejipanga kuibua miradi
ambayo itakuwa chachu na fursa kubwa kwao hasa katika miradi ya kilimo ambayo taasisi yetu inatarajia kuanzisha mashamba darasa katika kila halmashauri.
"Nina amini vijana wakipewa nafasi kubwa ya kujitegemea itakuwa
mkombozi kwa wao kujiondoa kifikra na kujipambanua zaidi kimaendeleo kuanzia
mtu mmoja mmoja na jamii inayowazunguka kiujumla," alisema Shabani.
Mhasibu wa Taasisi hiyo Mkoa wa Singida, Hadija Misanga, alisema pamoja na
mipango yote hiyo alisema wana programu ya kutoa mafunzo kwa vijana wenye umri
wa chini ili kujua nini maana ya uongozi na kuwafanya baadae wawe viongozi.
No comments:
Post a Comment