HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 18, 2023

TAKUKURU KYERWA YAPONGEZA MADIWANI

Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU Wilayani Kyerwa Wilson Mwapwele akizungumzia katika kikao cha baraza la madiwani.



Na Lydia Lugakila, Kyerwa

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera imelipongeza Baraza la madiwani la Halmashauri hiyo kutokana na kutoa ushirikiano mkubwa na kuiunga mkono Program mpya ya kuzuia na kupambana na Rushwa iitwayo TAKUKURU RAFIKI.

Akielezea hatua hiyo Mkuu wa Taasisi hiyo Wilson Mwapwele amesema tangu waitambulishe program hiyo mpya na kuikabidhi hivi karibuni kwa Halmashauri hiyo wamepata ushirikiano mkubwa toka kwa baadhi ya madiwani ambapo wamezifikia takribani kata nne za Wilaya hiyo huku Watendaji waliopo katika ngazi za kata  wakitoa ushirikiano wa kutosha.

"Nipende kuwashuru madiwani wa kata za Kakanja, Isingiro, Kaisho na Nkwenda kwa ushirikiano mliouonyesha juu ya program hii naahidi tutaendelea kwenda katika kata nyingine ili kubaini changamoto" alisema Mwapwele.

Amesema Program hiyo ya TAKUKURU RAFIKI ilibuniwa na Taasisi hiyo ili kusaidia kujenga ukaribu na urafiki wenye tija na wadau na imewekwa kwenye mpango mkakati wa TAKUKURU ambao umeanza kutumika mwaka 2020/2023 na unatarajiwa kuisha 2025/2026 lengo likiwa ni kuzuia vitendo vya Rushwa kabla havijatokea.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Taasisi amewawahimiza Viongozi wa Halmashauri hiyo kuwa washiriki namba moja katika kukemea vitendo vya Rushwa hata katika matendo mengine ya jinai.

Hata hivyo ameongeza kuwa Kelele nyingi zinazopigwa ni za ubadhilifu katika ngazi za kata na mitaani huku akiwasisitiza zaidi katika mapambano dhidi ya Magendo ya Kahawa.

No comments:

Post a Comment

Pages