Na John Marwa
KOCHA Mkuu wa Mashujaa FC, Abdallah Mohammed ‘Bares', amesema ataingia na mfumo mwingine katika mchezo wao wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold FC.
Mashujaa FC wanahitaji kuendelea kufanya vizuri katika mchezo wa pili utakaopigwa Jumatatu ya Agosti 21, 2023 wakiwakaribisha Geita Gold FC ambayo inayonolewa na kocha Hemed Morocco, mechi itakayopigwa uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Mechi hiyo itakuwa ya mvuto mkubwa kwa sababu ya makocha wa timu zote kufahamiana vizuri kimbinu kwa kuwa wanatoka Visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Habari Mseto Bares amesema baada ya kufanikiwa kupata ushindi mechi ya kwanza ya Ligi dhidi ya Kagera Sugar wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo huo kuelekea mechi yao dhidi ya Gaita Gold FC.
Amesema katika mechi ijayowataingia na mfumo tofauti na mechi ya kwanza kwa kuongeza nguvu zaidi safu ya ushambuliaji kwa sababu anafahamu mbinu za Kocha wa Geita Gold FC, Morocco.
“Hii mechi yetu itakuwa ya ushindani mkubwa naamini mbinu zitatawala zaidi katika mchezo huo kwa kuwa kocha wa Geita Gold FC , Hemed Morocco tunatoka sehemu mmoja na kila mmoja wetu anafahamu ubora wa mwenzake katika ufundi.
"Utakuwa mchezo mzuri, ninategemea kufanya mabadiliko ya kikosi lakini pia kuongeza watu mbele kulingana na ubora wa wapinzani wetu Geita Gold FC katika kila eneo na tunahitaji kushinda mechi hiyo,” alisema Bares.
Ameongeza kuwa anaimani na timu yake kufanya vizuri kwa msimu wa 2023/24 wa ligi, kwa kuwa wamekuja kuonyesha ushindani na sio kuja kushiriki na kushuka kwa sababu malengo yao ni kuona wanamaliza wakiwa kwenye nafasi tano za juu.
August 20, 2023
Home
Unlabelled
KOCHA BARES AMJIA KIVINGNE HEMED MOROCCO
KOCHA BARES AMJIA KIVINGNE HEMED MOROCCO
Share This

About HABARI MSETO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Author Details
Ut wisi enim ad minim veniam, quis nostrud exerci tation ullamcorper suscipit lobortis nisl ut aliquip ex ea commodo consequat. Duis autem vel eum iriure dolor in hendrerit in vulputate velit esse molestie consequat.
No comments:
Post a Comment